Tuesday 19 May 2009

Werder & Shakhtar kesho kucheza FAINALI ya UEFA CUP Istanbul, Turkey

  • =HII NI FAINALI YA MWISHO UEFA CUP
  • =MSIMU UJAO KUITWA 'UEFA EUROPA LEAGUE'
Klabu ya Bundesliga huko Ujerumani Werder Bremen na Shakhtar Donetsk kutoka Ukraine kesho usiku wanapambana kwenye Fainali ndani ya Uwanja wa Klabu ya Uturuki Fernebahce uitwao Sukru Saracoglu Stadium huko Istanbul, Uturuki kuwania Kombe la UEFA.

Kwenye Nusu Fainali Werder Bremen waliwabwaga wenzao wa Ujerumani Hamburg kwa goli la ugenini baada ya mechi zao mbili kumalizika kwa jumla ya bao 3-3.
Shakhtar Donetsk aliwatoa wenzao wa Ukraine Dynamo Kiev kwa jumla ya bao 3-2 kwenye mechi zao mbili za Nusu Fainali.
Pambano la kesho ni la kihistoria kwani hii ndio Fainali ya mwisho ya Kombe la UEFA baada ya kushindaniwa kwa miaka 38.
Kamati Kuu ya UEFA iliamua kuubadilisha mfumo wa Kombe hili kuanzia msimu ujao wa 2009/10 na pia kuupa jina jipya pamoja na Wadhamini wapya.
Mashindano haya ya UEFA CUP kuanzia msimu ujao yatachezwa kwa mtindo wa Makundi kwa mechi za nyumbani na ugenini ukifanana na mfumo wa UEFA CHAMPIONS LEAGUE. Jina jipya la mashindano hayo litakuwa 'UEFA EUROPA LEAGUE.'

No comments:

Powered By Blogger