Saturday 23 May 2009


BUNDESLIGA: WOLFSBURG WANYAKUA UBINGWA UJERUMANI KWA MARA YA KWANZA!!

Klabu ya Ujerumani Wolfsburg leo ikiwa Uwanja wa nyumbani Volkswagen Arena wameinyuka Werder Bremen mabao 5-1 na kuuchukua Ubingwa wa Ligi ya Ujerumani, Bundesliga, kwa mara ya kwanza katika historia yao. Magoli ya Wolfsburg yalifungwa na Misimovic dakika ya 5, Grafite mabao mawili, dakika ya 15 na 56, Prodl [kajifunga mwenyewe] dakika ya 26 na Dzeko dakika ya 74. Bao la Werder Bremen lilifungwa na Diego.

Nafasi ya pili imechukuliwa na Timu Kongwe Bayern Munich waliowafunga Vfb Stuttgart mabao 2-1. Licha ya kufungwa, Stuttgart wameshika nafasi ya 3 huku Hertha Berlin nafasi ya 4.
Mechi za leo za Bundesliga ndizo zilikuwa mechi za mwisho za msimu wa Ligi.

No comments:

Powered By Blogger