Thursday 7 May 2009

NI VURUGU BAADA YA CHELSEA KUTUPWA NJE!!
WACHEZAJI CHELSEA WALALAMIKIA NJAMA ZA KUZUIA ENGLAND KUWA NA TIMU 2 FAINALI!!

Wachezaji wa Chelsea wakiongozwa na Nahodha John Terry, Michael Ballack na Didier Drogba walimwandama Refa Tom Henning Ovrebo kutoka Norway wakilalamika uamuzi wake wa 'kuwanyima' penalti kadhaa baada ya Wachezaji wa Barcelona kuonekana wakiushika mpira ndani ya boksi.
Ballack alionekana akimshika Refa huyo huku Drogba akionekana mwenye ghadhabu akizuiwa na walinzi kumvamia na alibaki kuonyesha kidole na kufoka.
Nahodha wa Chelsea John Terry alilamika sana: 'Ni uamuzi mbovu! Nashangaa UEFA wanaweka Waamuzi dhaifu kwenye mechi kubwa! Tumekosa kuingia fainali kwa uamuzi mbovu!! Tizama mechi ya jana Darren Fletcher anaikosa Fainali kwa uamuzi mbovu!! Drogba hakufanya kosa ni haki kabisa kulalamika!!'
UEFA imesema inachunguza matukio hayo.
Lakini Meneja wa Chelsea, Guus Hiddink, ametetea vitendo hivyo kwa kusema ni kawaida damu kuchemka baada ya mechi na hakuna Mchezaji wake yeyote aliemvaa Refa Ovrebo ingawa yeye binafsi anashangaa kunyimwa penalti 3 au 4. Alipoulizwa kuhusu baadhi ya malalamiko ya Wachezaji wake waliosikika wakimpigia kelele Refa kwamba hizo ni njama za UEFA kuzuia Fainali ya Timu za England pekee, Hiddink alikataa kuamini kama kuna njama.
Manchester United waliingia Fainali juzi baada ya kuwatoa Arsenal.
MAN U WAWASILISHA RUFAA UEFA KUTENGUA KADI NYEKUNDU YA FLETCHER!!
Manchester United wamepeleka malalamiko yao rasmi kwa UEFA kuomba kuitengua Kadi Nyekundu aliyopewa Kiungo Darren Fletcher alietuhumiwa na Refa Roberto Rosetti kumchezea faulo Cesc Fabregas ndani ya boksi na Arsenal kupewa penalti iliyofungwa na Robin van Persie kwenye mechi ya juzi huko Emirates Stadium ambayo Man U waliwafunga Arsenal 3-1 na kuingia Fainali ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE.
Kanuni za UEFA zinazuia rufaa za aina hiyo lakini Man U wameipeleka isikilizwe kwa 'misingi ya kibinadamu.'

2 comments:

Anonymous said...

huyo drogba asuburi kuondoka chelse nimeona heading moja ktk moja ya magazeti ya UK Isemayo "get Drogba out of here" hebu tupe kwa kina nini kinaendelea juu yake

Anonymous said...

ok, mdau ntakupasha nikipata za uhakika si umbea!!!

Powered By Blogger