SPAIN BINGWA WA DUNIA!!!
Ilichukua muda wa nyongeza, dakika ya 116, kwa Iniesta kuipatia Spain bao la ushindi, baada ya dakika 90 za mpira usiokuwa na hadhi ya Fainali ya Kombe la Dunia kwa rafu na uongo wa kujirusha ovyo uliomfanya Refa Howard Webb toka England awe na wakati mgumu wa kuchagua Kadi ipi atoe na kufanya zitoke Kadi nyingi kupita Fainali yeyote ile.
Kila Mtu alijua Kadi Nyekundu itatolewa dakika yeyote na kweli ilitoka dakika ya 110 hivi kwa Heitinga wa Holland kupata Kadi ya Njano ya pili.Ni mechi iliyokuwa na nafasi chache za wazi ingawa Holland walipata mapema nafasi mbili ‘klia’ kupitia Robben na Spain kupitia Fabregas.
Timu:
SPAIN: Casillas, Sergio Ramos, Pique, Puyol, Capdevila, Busquets, Alonso, Xavi, Iniesta, Pedro, Villa.
Akiba: Valdes, Albiol, Marchena, Torres, Fabregas, Mata, Arbeloa, Llorente, Javi Martinez, Silva, Jesus Navas, Reina.
HOLLAND: Stekelenburg, Van Der Wiel, Heitinga, Mathijsen, Van Bronckhorst, Van Bommel, De Jong, Sneijder, Robben, Kuyt, van Persie.
Akiba: Vorm, Boulharouz, Ooijer, De Zeeuw, Braafheid, Elia, Schaars, Babel, Afellay, Huntelaar, Van der Vaart, Boschker.
No comments:
Post a Comment