CHEKI: www.sokainbongo.com
Ole amwaga sifa kwa Forlan
Shujaa Veterani wa Manchester United ambae sasa ni Meneja wa Timu ya Rezevu huko Old Trafford, Ole Gunnar Solskjaer, amesema hakushangazwa kwa Diego Forlan kushinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa Kombe la Dunia 2010 huko Afrika Kusini.
Ole alikuwepo wakati Staa huyo wa Uruguay anaingia Man United 2002 na kuondoka 2004 ambako alicheza mechi 63 na kufunga bao 10.
Ole Gunnar Solskjaer amenena: “Alipokuwa hapa Diego alikuwa mzuri. Bahati mbaya wakati huo tulikuwa na Ruud van Nistelrooy akifunga magoli kibao! Na Scholes alikuwa akicheza nyuma tu ya Ruud na yalitengenezwa magoli mengi sana. Na mimi pia nilikuwa wakati mwingine nacheza kama patna wa Ruud. Hayo yote yalimfanya yeye asipate nafasi za kucheza!”
Lakini Solskjaer amekiri Diego Forlan alikuwa Mchezaji mzuri ambae hata Sir Alex Ferguson alikubali aondoke kwenda Spain kwa shingo upande.
Bafana ina Kocha mpya
Msaidizi wa Kocha toka Brazil wa Timu ya Afrika Kusini, Carlos Alberto Parreira, Pitso Mosimane, ameteuliwa kuwa Kocha mpya wa Bafana Bafana kwa Mkataba wa Miaka minne.
Ni Parreira aliewashawishi Chama cha Soka kumteua Mosimane kama Kocha na sasa kazi kubwa mbele yake ni kuiwezesha Afrika Kusini kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika zitakazochezwa huko Gabon na Equatorial Guinea kwa pamoja Mwaka 2012 na zile zinazofuata 2013 huko Libya pamoja na kuiingiza Bafana Bafana Fainali za Kombe la Dunia 2014 huko Brazil.
Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitachezwa mfululizo 2012 na 2013 kwa vile mfumo utabadilika na kuanzia 2013 zitakuwa zikichezwa Miaka tasa [kila baada ya Miaka miwili] ili zisigongane na Fainali za Kombe la Dunia.
Mosimane amewataka wasaidizi waliokuwa chini ya Parreira kutoka Brazil wabaki ili kumsaidia.
Wasaidiza hao ni Jairo Leal na Francisco Gonzalez.
No comments:
Post a Comment