Thursday 25 March 2010

Bifu la Mancini v Moyes!!!
Mameneja wa Manchester City, Roberto Mancini, na wa Everton, David Moyes, huenda wakakabiliana na Pilato wa FA baada ya kufarakana wakati wa mechi ya Ligi Kuu hapo jana Uwanjani City of Manchester, mechi ambayo Everton waliinyuka Man City 2-0.
Sakata hilo lilitokea mpira ulipotoka nje ya uwanja na Moyes kuushika huku akigonja kubadilisha Mchezaji na ndipo Mancini akamvaa na kutaka kumpora mpira na ndipo mshikemshike ukaanza na kulazimu Refa wa Akiba Howard Webb na Walinzi kuwatenganisha.
Mameneja hao wawili wakatolewa nje ya Uwanja na Refa.
Alipohojiwa baada ya mechi, Mancini alijaribu kulipoza tukio hilo na kusema ameshaongea na kuomba radhi kwa mwenzake Moyes na mambo yote yamekwisha.
Nae Moyes amedai tukio hilo ni dogo na ameshangazwa mno kutolewa nje na Refa.
Katika mechi hiyo mabao ya Everton yalifungwa na Tim Cahill na Mikel Arteta.

No comments:

Powered By Blogger