Friday 26 March 2010

Chelsea yakumbwa na Majeruhi kibao!!
Wamebakiwa na Masentahafu wawili tu!
Chelsea wanaowania Ubingwa wakiwa nyuma ya vinara wa Ligi Kuu Manchester United kwa pointi moja tu wamepata pigo kwenye mechi ya jana ya Ligi waliyowabamiza Portsmouth 5-0 baada ya Beki wao Rivardo Carvalho kuumia.
Carvalho, miaka 31, aliumia enka na huenda akafanyiwa opersheni ambayo itamweka nje kwa zaidi ya mwezi.
Kuumia kwa Carvalho kumeifanya Chelsea ibakiwe na Masentahafu wawili tu, Mbrazil Alex na Nahodha John Terry, kwani Mchezaji mwingine ambae hucheza Sentahafu, Branislav Ivanovic, aliumia Jumapili iliyopita walipotoka sare na Blackburn bao 1-1 na inasemekana atakuwa nje kwa muda mrefu.
Majeruhi wengine wa muda mrefu Klabuni Chelsea ni Beki wa kushoto Ashley Cole [enka], Michael Essien [goti] na Jose Bosingwa [enka].
Jumamosi hii inayokuja, Chelsea wapo kwenye Ligi Kuu na wanacheza na Aston Villa, kisha Jumamosi inayofuata, Aprili 3, wako Old Trafford kucheza na Manchester United kwenye Ligi Kuu na Aprili 10 wako Wembley kucheza Nusu Fainali ya Kombe la FA watakapoikwaa Aston Villa.
Scholes ataka ushindi mechi 7 ili kuwa Bingwa!!!
Paul Scholes ana imani kubwa yeye na wenzake Manchester United wana uwezo wa kushinda mechi zote 7 zilizobaki za Ligi Kuu na hivyo kutetea taji lao la Ubingwa kwa mara ya 4 mfululizo na hivyo kuweka rekodi kwa kuwa Timu ya kwanza kutwaa Ubingwa mfululizo mara 4.
Pia, mpaka sasa Manchester United na Liverpool ndizo zinafungana kwa kuchukua Ubingwa mara 18 zikiwa ndio zilizoutwaa mara nyingi.
Katika mechi hizo 7 zilizosalia zipo mechi na Chelsea, Manchester City na Tottenham lakini Scholes anasema: “Mechi na Chelsea ni kubwa na lazima tushinde! Tunao Wachezaji bora ambao washawahi kuwa kwenye hali hii hivyo wanajua wajibu wao!”
Scholes akaongeza: “Huwezi ukawatoa kwenye hesabu Arsenal hasa kwa mechi zao zilizobaki! Washacheza na Timu kubwa zote na watakuwa na imani watashinda mechi zao! Lakini sisi tunajua Ubingwa uko mikononi mwetu! Tukishinda mechi zetu zote ni Mabingwa!”
MSIMAMO LIGI KUU England KWA TIMU ZA JUU:
1. Man United mechi 31 pointi 69
2. Chelsea mechi 31 pointi 68
3. Arsenal mechi 31 pointi 67
4. Tottenham mechi 30 pointi 55
MECHI ZILIZOSALI KWA VIGOGO WATATU: Arsenal, Chelsea & Man United
ARSENAL
Machi 27=Birmingham v Arsenal
Aprili 3=Arsenal v Wolves
Aprili 10=Tottenham v Arsenal
Aprili 18=Wigan v Arsenal
Aprili 24=Arsenal v Man City
Mei 1=Blackburn v Arsenal
Mei 9=Arsenal v Fulham
CHELSEA
Machi 27=Chelsea v Aston Villa
Aprili 3=Man United v Chelsea
Aprili 13=Chelsea v Bolton
Aprili 17=Tottenham v Chelsea
Aprili 25=Chelsea v Stoke
Mei 1=Liverpool v Chelsea
Mei 9=Chelsea v Wigan
[FAHAMU=Aprili 10 Chelsea v Aston Villa (Nusu Fainali FA CUP, Wembley Stadium)
MAN UNITED
Machi 27=Bolton v Man United
Aprili 3=Man United v Chelsea
Aprili 11=Blackburn v Man United
Aprili 17=Man City v Man United
Aprili 25=Man United v Tottenham
Mei 1=Sunderland v Man United
Mei 9=Man United v Stoke

No comments:

Powered By Blogger