Sunday 21 March 2010

Wenger atabiri Ubingwa baada ya kuipiga West Ham 2-0!!
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger anaamini Timu yake inao ubavu na ubora wa kutwaa Ubingwa Ligi Kuu na ametamka hivyo mara tu baada ya kuwafunga vibonde West Ham bao 2-0 hapo jana huku wakicheza Mtu 10 tu baada ya Beki wao Thomas Vermaelen kulambwa Kadi Nyekundu.
Ushindi huo umeifanya Arsenal iongoze Ligi kwa vile tu Chelsea na Manchester United hazikucheza Jumamosi na mechi zao zipo Jumapili.
Katika ushindi huo, mabao ya Arsenal yalifungwa na Denilson na Cesc Fabregas kwa penalti.
Wakati Vermaelen anatolewa, West Ham walipewa penalti iliyopigwa na Alessandro Diamanti na kuokolewa na Kipa wa Arsenal Manuel Almunia.
Wenger ametamba: “Tuna nafasi nzuri msimu huu!”
Kimahesabu na kitabuni, Arsenal wamesaliwa na mechi ‘mchekechea’ ukilinganisha na Wapinzani wao Chelsea na Man United ambao wana mechi kati yao wenyewe wakati Arsenal ameshamaliza mechi zote na Vigogo Chelsea, Man United na Liverpool.

No comments:

Powered By Blogger