Sunday 21 March 2010

BIGI MECHI: Man United v Liverpool
Jumapili, Machi 21 Uwanja: Old Trafford Saa: 10 na Nusu jioni, saa za bongo
• Liverpool imeshinda Mechi 3 mfululizo, Vidic alambwa Kadi Nyekundu Mechi zote hizo 3!!!
Timu hizi zilikutana mara ya mwisho Mwezi Oktoba mwaka jana na Liverpool walishinda 2-0 na hiyo ikiwa ni mara ya 3 mfululizo kwa Liverpool kuifunga Manchester United.
Msimu uliokwisha, Liverpool walishinda mechi zote mbili za Ligi kwa 2-1 huko Anfield na 4-1 uwanjani Old Trafford.
Katika mechi zote hizo 3 ambazo Manchester United walifungwa, Beki wao Nemanja Vidic amekuwa akitolewa kwa Kadi Nyekundu na hivyo kulainisha ushindi kwa Liverpool.
Mbali ya kuikandya FA kwa maamuzi yake yanayoikandamiza Man United hasa kwenye masuala ya nidhamu ikizingatiwa kufungiwa kwa Mchezaji wake Rio Ferdinand mechi 4 wakati Steven Gerrard na Javier Mascherano wa Liverpool hawaadhibiwi chochote kwa makosa yaliyofanana na ya Rio, Sir Alex Ferguson, Meneja wa Manchester United, ametamka: “Tunajua wao Liverpool siku zote bahati huanguka kwao! Kwa hilo wanafanya vizuri! Labda siku moja bahati itakuwa yetu!”
Akizungumzia kutolewa kwa Kadi Nyekundu Beki wake Nemanja Vidic katika mechi 3 mfululizo na Liverpool ambazo Liverpool walishinda mechi zote hizo 3, Ferguson alisema: “Zile Kadi 2 Nyekundu alizopata Anfield ni sababu ya shinikizo la kelele za Mashabiki na Wachezaji wa Liverpool! Nimeziangalia tena zote! Sio sahihi hata kidogo!”
Katika mechi ya Jumapili, Liverpool wana listi ndogo ya majeruhi akiwemo Difenda Martin Skrtel pekee ingawa Albert Riera hatakuwepo kutokana na suala lake la nidhamu ndani ya Klabu.
Man United wana listi ndefu ya majeruhi wakiwemo Ritchie De Laet, Wes Brown, Rafael da Silva, Michael Owen, Anderson, John O’Shea na Owen Hargreaves.
Ryan Giggs, aliekuwa akiuguza mkono uliovunjika, huenda akacheza.
VIKOSI VINATEGEMEWA KUWA:
Manchester United (4-4-2): Van der Sar; Neville, Ferdinand, Vidic, Evra; Valencia, Carrick, Scholes, Nani; Berbatov, Rooney.
Liverpool (4-5-1): Reina; Johnson, Carragher, Agger, Insua; Maxi, Aquilani, Mascherano, Babel; Gerrard, Torres.
Refa: Howard Webb. [Amechezesha Mechi 21 Kadi Nyekundu 3 Njano 77]
TAKWIMU YA MECHI: Zimetolewa Kadi Nyekundu 6 katika Mechi 6 za mwisho za Ligi kati ya Timu hizi.

No comments:

Powered By Blogger