Monday 22 March 2010

Pompey na balaa jingine!!!
• Yashindiliwa Faini Pauni Milioni 1!!!
Wasimamizi wa LIGI KUU England wameipiga Klabu ya Portsmouth Faini ya Pauni Milioni 1 kwa kukiuka sheria na taratibu mbalimbali za Ligi Kuu zikiwemo kuchelewesha mishahara ya Wachezaji, kutokulipa Ada za Uhamisho na kadhalika.
Portsmouth ipo kwenye ukata mkubwa na imenusurika kufilisiwa baada ya kuamuliwa iwekwe chini ya Msimamizi maalum na hilo pia, ingawa ni kuiokoa Klabu isife, ni kinyume cha taratibu za Ligi Kuu na limesababisha ikatwe pointi 9.
Portsmouth wapo mkiani mwa msimamo wa Ligi Kuu na wapo hatarini kushushwa Daraja kwani wapo pointi 11 nyuma ya Timu iliyo juu yao huku wakiwa wamebakiwa na mechi 8.
Faini hiyo ya Pauni Milioni 1 inategemewa kuchukuliwa toka mapato yao ya kutoka Makampuni ya TV.

No comments:

Powered By Blogger