MECHI ZA LEO JUMATANO Machi 24:
FA CUP
Tottenham v Fulham [Marudio ya Robo Fainali baada ya kutoka sare 0-0]
LIGI KUU
Portsmouth v Chelsea
Man City v Everton
Blackburn v Birmingham
Aston Villa v Sunderland
=======================================================================
MSIMAMO LIGI KUU England:
1. Man United mechi 31 pointi 69
2. Arsenal mechi 31 pointi 67
3. Chelsea mechi 30 pointi 65
4. Tottenham mechi 30 pointi 55
------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
5. Man City mechi 29 pointi 53
6. Liverpool mechi 31 mechi 51
7. Aston Villa mechi 29 pointi 50
8. Everton mechi 30 pointi 45
9. Birmingham mechi 30 pointi 44
10. Fulham mechi 30 pointi 38
11. Stoke mechi 30 pointi 36
12. Blackburn mechi 30 pointi 35
13. Sunderland mechi 30 pointi 34
14. Bolton mechi 31 pointi 32
15. Wolves mechi 31 pointi 31
16. Wigan mechi 31 pointi 31
17. West Ham mechi 31 pointi 27
------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
18. Burnley mechi 31 pointi 24
19. Hull mechi 30 pointi 24
20. Portsmouth mechi 30 pointi 13
======================================================================
Wachezaji Pompey waokoa ajira za Wafanyakazi!!
Imebainika Wachezaji wa Klabu taabani Portsmouth, ambayo iko mkiani Ligi Kuu, imekatwa pointi 9 na Ligi Kuu na yenye ukata mkubwa wa fedha, wamejichangisha ili kuokoa ajira za Wafanyakazi wanne waliokuwa hatarini kutimuliwa muda wowote ule ili kuungana na wengine 85 waliopunguzwa hivi karibuni.
Lakini Wachezaji wa Timu hiyo, wakiongozwa na Nahodha Kipa David James, wameamua kuchanga Pauni 1500 kila mtu ili kuwanusuru Wafanyakazi hao wanne ambao ni Msimamizi wa Matengenezo wa Uwanja, Mchua Musuli na wengine wawili.
Meneja wa Portsmouth, Avram Grant, akithibitisha taarifa hizo, amesema: “Wachezaji, mimi mwenyewe na wengine, wametoa mchango wao kwa moyo mkunjufu. Hawa Wafanyakazi wanne wako hapa kabla yetu na watakuwa hapa hata tukiondoka!”
Mmoja wa Wafanyakazi hao, Tug Wilson, ambae ndie Msimamizi wa Uwanja, amenena: “Siku hizi tunasikia mengi mabaya kuhusu Wachezaji lakini kitendo cha Wachezaji hawa ni utu na ni kitu cha kushangaza!”
Avram Grant ameongeza: “Tug yuko hapa miaka mingi, ana kazi ngumu kuanzia asubuhi hadi usiku na mshahara mdogo. Nina furaha atabaki. Ikifika wakati Klabu inakosa utu wake basi imekwisha!”
Arsenal haina ubavu kuwa Mabingwa, adai Arshavin!!!
Andrey Arshavin, Fowadi wa Arsenal kutoka Urusi, ana hofu kwamba Arsenal haina ubavu kwa Kikosi kilichopo kuweza kubeba Makombe msimu huu.
Msimu huu, Arsenal bado wapo kwenye kinyang’anyiro cha Ligi Kuu England ambako wako nafasi ya pili nyuma ya Manchester United na pia wamo Robo Fainali UEFA CHAMPIONS LIGI watakapowavaa Mabingwa Watetezi Barcelona.
Lakini Kikosi hicho cha Arsene Wenger kinakabiliwa na matatizo makubwa ya ukosefu wa Kikosi kikubwa na hasa wanapokuwepo majeruhi wengi.
Arshavin amesema: “Maoni yangu ni kuwa tunahitaji Wachezaji wengine wengi. Mwishoni mwa Msimu uliokwisha tuliuza Wachezaji wawili na kununua mmoja tu. Sasa tumewapoteza Mastaa Van Persie, Kieran Gibbs na Aaron Ramsey ambao wameumia!”
Arshavin ameendelea kudai bila ya Wachezaji wengi ni rahisi sana kwa wapinzani wao kuwasoma na kujua mbinu na mikakati yao na hivyo wanapata uwezo wa kuwakaba kirahisi na kuwashambulia.
West Ham 1 Wolves 3
Wolves wamepiga hatua kubwa ili kujinasua mkiani walipowafunga West Ham katika mechi pekee ya Ligi Kuu Jumanne usiku kwa mabao 3-1 Uwanjani Upton Park.
Mabao ya Wolves yalifungwa na Kevin Doyle, Ronald Zubar na Mathew Jarvis.
Bao pekee la West Ham lilipachikwa na Guillermo Franco.
Ushindi huo umeipandisha Wolves nafasi moja na wako nafasi ya 15 wakiwa na pointi 31 kwa mechi 31.
West Ham wamebaki nafasi ya 17 wakiwa na pointi 27 kwa mechi 31 na wako juu ya Timu za 18 na 19, Burnley na Hullm City, kwa pointi 3 tu.
Portsmouth wako nafasi ya mwisho, nafasi ya 20, na wana pointi 13 tu baada ya kunyang’anywa pointi 9 na Ligi Kuu.
Timu zitakazoshika nafasi za 18, 19 na 20 mwishoni mwa msimu ndizo hushushwa Daraja.
No comments:
Post a Comment