Tuesday 23 March 2010

Rufaa ya Vermaelen yatupwa!!
Leo FA imetupilia mbali rufaa ya Arsenal kupinga Kadi Nyekundu aliyopewa Beki wao Thomas Vermaelen siku ya Jumamosi kwenye mechi ya Ligi Kuu waliyowafunga West Ham 2-0 na hivyo haruhusiwi kucheza mechi ya Ligi ya Jumamosi ijayo Arsenal atakapokuwa ugenini kucheza na Birmignham.
Refa Martin Atkinson alimtoa Vermaelen alipomchezea Guillermo Franco faulo alipokuwa akienda kufunga na hivyo kufungiwa mechi moja.
Itabidi Wakongwe Sol Campbell na Mikel Silvestre wazibe mapengo ya Vermaelen na Gallas, ambae ni majeruhi, kwa mechi hiyo ya Jumamosi.
LIGI KUU Leo: West Ham v Wolves
Uwanjani Upton Park, leo usiku West Ham watawaalika wenzao Wolves katika mechi ya Ligi Kuu inayozikutanisha Timu iliyo nafasi ya 16, Wolves, na ile iliyo nafasi ya 17, West Ham, huku Wolves ana pointi 28 na West Ham wana pointi 27.
Hii ni mechi muhimu mno kwa Timu zote mbili hasa ukizingatia wao wako juu tu ya Timu 3 za mwisho, Burnley, Hull City na Portsmouth, ambazo ndizo ziko eneo la hatari la kushushwa Daraja na Timu za Burnley na Hull zina pointi 24 kila mmoja.

No comments:

Powered By Blogger