Sunday 21 March 2010

Man United yaikata ngebe Liverpool!!
Leo katika Uwanja wa Old Trafford Manchester United wameupiga stopu uteja kwa Liverpool na kuwatandika Mahasimu wao hao bao 2-1 na kutwaa uongozi wa Ligi Kuu kutoka kwa Arsenal walioushika tangu jana.
Sasa Man United ana pointi 69 akifuatiwa na Arsenal mwenye pointi 67 na Chelsea ni wa 3 akiwa na pointi 64 huku ana mechi mbili mkononi.
Liverpool ndio walioanza vyema mechi hii baada ya Fernando Torres kuwapa bao kwa kichwa dakika ya 5 tu baada ya krosi ya Kuyt.
Man United walisawazisha dakika ya 12 kwa bao la Wayne Rooney aliefunga baada ya penalti yake kuokolewa na Kipa Reina na mpira kumrudia Rooney ambae hakufanya kosa kwa mara ya pili.
Penalti hiyo ya Rooney ilisababishwa na Mascherano kumchezea rafu Valencia na Refa kuamuru penalti.
Hadi mapumziko mabao yalikuwa 1-1.
Ndipo kwenye dakika ya 60 Ji-Sung Park alipofunga kwa kichwa cha kudaivu baada ya krosi ya Darren Fletcher.
Vikosi vilivyoanza:
Man Utd: Van der Sar, Neville, Ferdinand, Vidic, Evra, Valencia, Fletcher, Carrick, Park, Rooney, Nani.
AKIBA: Kuszczak, Berbatov, Giggs, Scholes, Rafael Da Silva, Jonathan Evans, Obertan.
Liverpool: Reina, Johnson, Carragher, Agger, Insua, Mascherano, Lucas, Kuyt, Gerrard, Maxi, Torres.
AKIBA: Cavalieri, Aquilani, Benayoun, Kyrgiakos, Babel, Ngog, Kelly.
REFA: Howard Webb

No comments:

Powered By Blogger