Monday 22 March 2010

WAFUNGAJI BORA LIGI KUU:
1. Rooney 26 [Man United]
2. Drogba 22 [Chelsea]
3. Bent 20 [Sunderland]
4. Defoe 17 [Tottenham]
5. Tevez 16 [Man City]
6. Torres 16 [Liverpool]
7. Fabregas 15 [Arsenal]
8. Saha 13 [Everton]
9. Lampard 12 [Chelsea]
10. Agbolanhor 11 [Aston Villa]
11. Berbatov 10 [Man United]
12. Adebayor 9 [Man City]
13. Arshavin 9 [Arsenal]
14. Carlton Cole 9 [West Ham]
15. Jerome 9 [Birmingham]
KWA UFUPI TU:
-Wenger kuhusu Van Persie:
Arsene Wenger ana matumaini kidogo kuwa Staa wake Robin van Persie huenda akaonekana tena uwanjani msimu huu baada ya kupata nafuu vizuri enka yake aliyofanyiwa operesheni baada ya kuumizwa Novemba mwaka jana akiichezea Nchi yake Uholanzi ilipokutana na Italia.
Wenger amesema hata akirudi tena mazoezini bado anahitaji si chini ya wiki 3 ili kuwa fiti na hiyo itamchukua hadi Mei.
Msimu wa Ligi unakwisha Mei 9.
-Allardyce na Fergie:
Sam Allardyce, Meneja wa Blackburn Rovers ambayo jana ilitoka sare 1-1 na Vigogo Chelsea, amesema sare hiyo si kwa ajili ya rafiki yake Sir Alex Ferguson wa Manchester United bali ni kwa ajili yao ili kujihakikishia usalama wao wa kutoshuka Daraja.
-Owen Hargreaves kupona:
Owen Hargreaves wa Manchester United huenda akarudi kwenye Kikosi cha kwanza mwezi ujao baada ya kucheza dakika 45 za kwanza za Kikosi cha Pili cha Man United kilichoifunga Burnley 2-0.
Sir Alex Ferguson amesema amefurahi mno kumwona Hargreaves uwanjani baada kuwa nje kwa Miezi 18 akiuguza magoti aliyofanyiwa operesheni.
-Robert Mancini:
Roberto Mancini, Meneja wa Manchester City kutoka Italia, anategemea Mchezaji wake Wayne Bridge atabadilisha uamuzi na kuichezea England baada ya kuisusa kutokana na kashfa ya John Terry kutembea na gelfrendi wake wa zamani.
Mancini anataka Bridge abadilishe uamuzi hasa kwa vile yeye anaamini sana kuwa England ina uwezo wa kunyakua Kombe la Dunia.
England ipo chini ya Mtaliana mwingine Fabio Capello ambae ameacha mlango wazi kwa Bridge kujiunga na England hasa baada ya Beki wa kutumainiwa Ashley Cole kuwa majeruhi wa muda mrefu na atakosekana kwenye Fainali za Kombe la Dunia.
-Rafa alia na penalti ya Man United:
Rafa Benitez wa Liverpool amedai Refa Howard Webb hakustahili kuwapa penalti Manchester United katika ushindi wao wa bao 2-1 hapo jana kwa vile Valencia alijiangusha.
Mikanda ya Video ilionyesha wazi Kiungo wa Liverpool Mascherano akimvuta jezi Valencia ingawa kitendo hicho kilianzia nje ya boksi na kuendelea hadi ndani ya penalti.
Wayne Rooney alipiga penalti hiyo lakini Kipa Reina aliokoa na mpira kurudi tena kwa Rooney aliefunga bao la kusawazisha.
Wakati huo huo, Sir Alex Ferguson amedai Mascherano alistahili kupewa Kadi Nyekundu na si Njano kama aliyopewa kwa faulo hiyo kwa Valencia kwa vile alikuwa mtu wa mwisho na alimzuia Valencia asiende kufunga.

No comments:

Powered By Blogger