Saturday, 27 March 2010

Bondeni Viwanja Bomba
Afrika Kusini jana imetangaza kuwa Viwanja vyote 10 vitakavyochezewa mechi za Fainali za Kombe la Dunia kuanzia Juni 11 hadi Julai 11 vimekamilika baada ya FIFA kumaliza ukaguzi wao wa mwisho uliochukua siku10.
Mkuu wa Kamati ya Maandalizi ya Afrika Kusini Danny Jordan amesema: “Tumetimiza ahadi yetu ya kuwa na Viwanja bora kabla Mashindano kuanza na tena tumetimiza hili kabla ya muda wake!”
Kati ya Viwanja hivyo 10, sita ni Viwanja vipya kabisa na vinne ni vya zamani vilivyokarabatiwa.
Pompey wanaamini wameonewa!
Meneja wa Portsmouth Avram Grant anamini kuwa Ligi Kuu wamekosea kwa jinsi walivyokuwa wakiwatendea hasa uamuzi wa kuwazuia kutosajili Wachezaji uliofanywa Oktoba mwaka jana na ambao uliondolewa siku chache kabla ya dirisha la uhamisho kufungwa mwezi Januari.
Pompey wanakabiliwa na ukata mkubwa na wako chini ya Msimamizi maalum kuwanusuru wasifilisike na kufa na hilo limewafanya FA kuwakata pointi 9 hivyo kuwafanya wang’ang’anie mkiani mwa Ligi na kushuka Daraja ni, pengine, lazima kwao.
Tatizo hilo la kutosajili limeifanya Pompey iwe na uhaba wa Wachezaji na Grant, ambayo Timu yake inacheza na Tottenham leo kwenye Ligi Kuu, amedai: “Tuna Wachezaji 13 au 14 tu kwa mechi na Tottenham! Hili ni tatizo la uamuzi wao waliotufanyia Januari! Hatuwezi kushindana na Tottenham!”
Mbrazil Sandro kutua Spurs
Tottenham imethibitisha kumsajili Mchezaji wa Kimataifa wa Brazil Sandro, miaka 21, kutoka Klabu ya Internacional ya Marekani ya Kusini kwa dau la Pauni Milioni 6 na atajiunga na Tottenham mwanzoni mwa Msimu ujao.
Sandro, ambae ni Kiungo, ameichezea Timu ya Brazil ya Vijana Chini ya Miaka 21 mara 8 na kucheza mechi moja kwenye Kikosi cha kwanza cha Brazil ilipocheza na Chile Septemba mwaka jana katika mechi za mchujo za Kombe la Dunia.
Gerrard akiri kiwango chini msimu huu!!
Nahodha wa Liverpool, Steven Gerrard, amekiri Msimu huu kiwango chake kimekuwa chini ya kawaida yake na hilo limeifanya hata Liverpool kuyumba.
Liverpool tayari wapo nje ya UEFA CHAMPIONS LIGI, FA CUP na kwenye Ligi Kuu nafasi wanayoipigania ni kumaliza nafasi ya 4 na hivyo kucheza UEFA Msimu ujao lakini hata nafasi hiyo inategemea matokeo ya Timu nyingine na haipo mikononi mwao.
Kinyang’anyiro pekee ambacho kipo mikononi mwao ni EUROPA LIGI ambako wako Robo Fainali na watacheza na Benfica ya Ureno mwezi Aprili.
Gerrard amekiri: “Fomu yangu msimu huu hainipi furaha! Sishtuki kwani najua ntabadilika!”

No comments:

Powered By Blogger