Saturday 27 March 2010

LIGI KUU: Chelsea yaangusha kipondo Stamford Bridge!!!!
• Chelsea 7 Aston Villa 1
• Arsenal yakwama!!
Chelsea imeifumua Aston Villa bao 7-1 kwenye mechi ya Ligi Kuu Uwanjani Stamford Bridge na hivyo kutwaa uongozi wa Ligi wakiwa na pointi 71 kwa mechi 32 lakini Manchester United, wenye pointi 69 kwa mechi 31, wanacheza muda mfupi ujao na Bolton na ushindi kwao utawafanya waipiku Chelsea na kushika hatamu.
Hadi mapumziko Chelsea walikuwa mbele kwa bao 2-1.
Mabao ya Chelsea yalifungwa na Lampard, bao 4 mbili za penalti, Malouda 2 na Kalou bao moja.
Bao la Aston Villa lilifungwa na John Carew.
Chelsea na Aston Villa zitakutana tena Uwanjani Wembley kwenye Nusu Fainali ya Kombe la FA hapo Aprili 10.
Nao Arsenal wamenasa kwenye nafasi yao ya 3 baada ya kwenda sare 1-1 na Birmingham katika Uwanja wa Mtakatifu Andrew.
Arsenal sasa wamecheza mechi 32 na wana pointi 68.
Arsenal ndio waliopata bao kwanza dakika ya 81 kwa mzinga wa Samir Nasri lakini kwenye dakika za lala salama, dakika ya 92, patashika langoni kwa Arsenal ilimbabatiza Straika wa Birmingham Kevin Phillips na Kipa Manuel Almunia akazembea katika kuokoa na mpira kutinga wavuni.
MATOKEO: Jumamosi, Machi 27
Birmingham 1 v Arsenal 1
Chelsea 7 v Aston Villa 1
Hull City 2 v Fulham 0
Tottenham 2 v Portsmouth 0
West Ham 0 v Stoke City 1
Wolves 0 v Everton 0

No comments:

Powered By Blogger