LIGI KUU: Wikiendi hii patamu!!!
RATIBA
Jumamosi, Machi 27
Birmingham v Arsenal
Bolton v Man United
Chelsea v Aston Villa
Hull City v Fulham
Tottenham v Portsmouth
West Ham v Stoke City
Wolves v Everton
Jumapili, Machi 28
Burnley v Blackburn
Liverpool v Sunderland
TATHMINI:
Bolton v Manchester United
Vinara wa Ligi Kuu Manchester United watasafiri hadi Bolton kuikwaa Bolton Wanderers huku wakiwania ushindi wao wa tano mfululizo kwenye Ligi Kuu na hivyo kuimarisha kiu yao ya kutwaa Ubingwa kwa mara ya 4 mfululizo.
Bolton hivi karibuni wamekuwa wakipata mafanikio ambayo yamewafanya waweke pengo la pointi 8 kati yao na zile Timu zilizo hatarini kuporomoka Daraja.
Birmingham v Arsenal
Ushindi wa Chelsea huko Portsmouth siku ya Jumatano umewafanya Arsenal warudishwe nyuma hadi nafasi ya 3 na hivyo ushindi huko ugenini Birmingham ni muhimu kwao.
Arsenal watakuwa bila ya Sentahafu waoThomas Vermaelen aliefungiwa.
Kwa Birmingham mechi hii ni muhimu hasa baada ya kupoteza mechi mbili zilizopita.
Chelsea v Aston Villa
Meneja wa Chelsea Carlo Ancelotti bila shaka atakuwa akiomba ule wakati mgumu kwao uwe umepita na hivyo kuifunga Timu ngumu Aston Villa iliyo nafasi ya 7 na inayowania nafasi muhimu ya 4 ili kucheza UEFA msimu ujao.
Katika mechi ya kwanza ya Ligi kati ya Timu hizi mbili, Aston Villa ndio waliibuka kidedea.
Tottenham v Portsmouth
Timu hizi zitakutana huko Wembley Aprili 11 kwenye Nusu Fainali ya FA CUP lakini kwa sasa kinyang’anyiro ni kiu ya Tottenham kuidhibiti nafasi ya 4 waliyokuwa nayo ili wacheze UEFA msimu ujao huku Portsmouth walio mkiani wakipigana kufa na kupona kutoshuka Daraja ingawa hilo sasa ni kudra ya Mungu tu hasa baada ya kupokwa pointi 9 na Ligi Kuu.
===================================================================
MSIMAMO LIGI KUU England:
1. Man United mechi 31 pointi 69
2. Chelsea mechi 31 pointi 68
3. Arsenal mechi 31 pointi 67
4. Tottenham mechi 30 pointi 55
---------------------------------------------------------------------------------------------
5. Man City mechi 30 pointi 53
6. Liverpool mechi 31 mechi 51
7. Aston Villa mechi 30 pointi 51
8. Everton mechi 31 pointi 48
9. Birmingham mechi 31 pointi 44
10. Blackburn mechi 31 pointi 38
11. Fulham mechi 30 pointi 38
12. Stoke mechi 30 pointi 36
13. Sunderland mechi 31 pointi 35
14. Bolton mechi 31 pointi 32
15. Wolves mechi 31 pointi 31
16. Wigan mechi 31 pointi 31
17. West Ham mechi 31 pointi 27
-----------------------------------------------------------------------------------------------
18. Burnley mechi 31 pointi 24
19. Hull mechi 30 pointi 24
20. Portsmouth mechi 31 pointi 13
========================================================================
West Ham v Stoke City
Baada ya kipigo cha 3-1 walichopewa na Wolves siku ya Jumanne, mechi hii ina maana kubwa sana kwa West Ham na hasa Meneja wao Zol hasa kufuatia manung'uniko ya Mashabiki wa West Ham.
West Ham wako pointi 3 tu juu ya Timu 3 za mwisho na ushindi ni kitu cha lazima kwao lakini Stoke City nao, ingawa wana afueni kidogo, katika mechi zao 10 zilizopita wameshinda mara mbili tu na hivyo wanahitaji kubadilika.
Hull City v Fulham
Hii ni mechi ya pili kwa Meneja mpya wa Hull, Ian Dowie, ya kwanza iliisha kwa kuchapwa na Portsmouth dakika za lala salama kwa bao 3-2.
Lakini hii ni mechi ngumu kwa Hull kwani wanakutana na kigaga Fulham ambao ndio kwanza wanatoka kwenye huzuni ya kubwagwa nje ya Kombe la FA walipotwangwa bao 3-1 na Tottenham hapo Jumatano katika mechi ya marudio.
Wolves v Everton
Wolves wanaikaribisha Everton ambayo imeingia kwenye ile ‘Ligi ndogo’ ya kuwania nafasi ya 4 kwani sasa wako pointi 3 nyuma ya wagombea wengine wa nafasi hiyo ya 4, Liverpool na Aston Villa.
Mafanikio katika mechi za hivi karibuni zimewafanya Wolves wajikite kwenye nafasi za usalama na matokeo mazuri dhidi ya Everton yatawafanya wajenge zaidi uhai wao.
Burnley v Blackburn
Hii ni mechi ya kwanza siku ya Jumapili na ni ya kufa na kupona kwa Burnley walio nafasi ya 18 wakiwa moja ya Timu 3 zilizo nafasi za kushushwa Daraja.
Kwa Blackburn, walio kwenye usalama mkubwa ukilinganisha na Burnley, hii ni mechi itakayozidi kuwakikishia usalama endapo watashinda
Liverpool v Sunderland
Wengi watakumbuka kipigo cha Liverpool toka kwa Sundeland katika mechi ya kwanza ya Ligi hasa baada ya goli la ushindi la Sunderland kufungwa na Darren Bent kwa msaada mkubwa wa “Bichi Boli”.
Liverpool ndio kwanza wanatoka kwenye kipigo cha 2-1 toka kwa Mahasimu wao wakubwa Manchester United na hivyo kuwayumbisha kwenye azma yao ya kuinyakua nafasi ya 4 ya Ligi ili wacheze UEFA msimu ujao na hivyo matokeo mazuri katika mechi hii ni muhimu.
Sunderland watataka kuendeleza wimbi la kutofungwa katika mechi yao ya 6 mfululizo.
No comments:
Post a Comment