Monday 22 March 2010

Chelsea wakwama Ewood Park!!
• Wapo nafasi ya 3!!
Leo katika mechi ya Ligi Kuu, nia ya Chelsea kupata pointi 3 na hivyo kuikaribia Manchester United ilitupwa nje na Timu ngumu Blackburn Rovers waliokuwa nyumbani Ewood Park na kulazimisha sare ya bao 1-1.
Sare hii ya Chelsea imezinufaisha sana Manchester United na Arsenal ambazo sasa zipo juu ya Chelsea huku Man United, ambae jana alimtandika Liverpool 2-1, akiongoza Ligi kwa kuwa na pointi 69 kwa mechi 31 na wa pili ni Arsenal akiwa na pointi 67 kwa mechi 31 na Chelsea ni wa 3 akiwa na pointi 65 kwa mechi 30.
Chelsea walikuwa ndio wa kwanza kupata bao kupitia Didier Drogba baada ya pande tamu la Nicholas Anelka.
Bao hilo lilidumu hadi mapumziko.
Kipindi cha pili El-Hadji Diouf aliisawazishia Blackburn baada ya krosi ya Michel Salgado.
Fulham 1 Man City 2
Huko Craven Cottage, Fulham wakiwa wametoka kwenye furaha ya kuitwanga Juventus 4-1 hapo juzi kwenye EUROPA LIGI, jana Jumapili wamepigwa bao 2-1 na Manchester City kwenye mechi ya LIGI KUU.
Mabao ya Man City yalifungwa na Roque Santa Cruz na Carlos Tevez.
Bao la Fulham lilifungwa kwa penalti na Danny Murphy baada ya Gareth Barry kuunawa mpira.

No comments:

Powered By Blogger