Tuesday 30 September 2008


KIPIGO CHA HULL CITY CHAMTIA KIWEWE WENGER!

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger ameweweseka na kipigo toka kwa timu mpya LIGI KUU Hull City walichokipata Emirates Stadium ambayo ni ngome ya Arsenal walipobandikwa bao 2-1 Jumamosi iliopita kwenye mechi ya LIGI KUU.
Wenger alipohojiwa baada ya mechi alihuzunika sana na kuweweseka kiasi cha kutojua ni timu gani iliyomfunga na akawa anaitaja ni West Bromwich Albion badala ya Hull City. Pengine hali hiyo ilijitokeza kwa sababu siku hiyo ya kipigo ilikuwa ni siku yake kuadhimisha miaka 12 tangu atue Arsenal.

Wenger sasa ameahidi shoka litaanguka kwa baadhi ya Wachezaji kwenye mechi ya leo wanayocheza hapohapo kwao Emirates Stadium leo saa 3 dakika 45 usiku, saa za bongo, watakapocheza na timu mahiri na ngumu ya Ureno FC Porto katika mechi ya KUNDI G ya mashindano ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE.

Katika mechi za kwanza za Kundi hili FC Porto iliifunga timu machachari ya Uturuki Fenerbahce bao 3-1 walipocheza Ureno. Arsenal walitoka chupuchupu huko Ukraine walipochomoa bao dakika za mwisho na kutoka sare ya 1-1 na waliokuwa wenyeji wao Dynamo Kiev.

Arsene Wenger ameahidi mabadiliko kwenye kikosi na inatumainiwa Samir Nasri na Mikael Silvestre wanaweza kuanza kwani wote sasa wamepona maumivu yao.

No comments:

Powered By Blogger