Friday 3 October 2008

UEFA CUP: EVERTON WATUPWA NJE, TOTTENHAM, ASTON VILLA NA PORTSMOUTH WASONGA MBELE!

Jana Timu kadhaa za Uingereza zilijitupa uwanjani katika mechi za marudiano za kuamua timu zipi zinaingia raundi ya makundi kugombea Kombe la UEFA.
Matokeo ni kama ifuatavyo:

Wisla Krakow 1-1 Tottenham

Tottenham wasonga mbele kwa jumla ya mabao 3-2 baada ya kushinda mechi ya kwanza 2-1.

Standard Liege 2-1 Everton

Everton wametupwa nje kwa jumla ya mabao 4-3. Mechi ya kwanza walitoka suluhu 2-2.

Man City 2-1 Omonia Nicosia

Man City wanasonga mbele kwa kushinda mechi zote mbili kwa mabao 2-1 kila moja.

Aston Villa 1-1 Litex Lovech

Aston Villa walishinda mechi ya kwanza kwa mabao 3-1 hivyo wameingia raundi nyingine kwa jumla ya mabao 4-2.

Guimaraes 2-2 Portsmouth

Portsmouth walishinda mechi ya kwanza kwa mabao 2-0 lakini kwenye mechi hii ya marudiano walipigwa 2-0 hadi dakika 90 zilipokwisha na kufanya timu ziwe sare kwa jumla ya magoli 2-2.
Ndipo muda wa nyongeza ukachezwa na Portsmouth wakamudu kurudisha kwa mabao yaliyofungwa na Mshambuliaji wao ‘ngongoti’ Peter Crouch na kufanya mechi iwe sare ya 2-2 lakini Portsmouth wamesonga mbele kwa jumla ya mabao 4-2.

No comments:

Powered By Blogger