Saturday, 4 October 2008

Ferguson aomba radhi kwa Ince

Wakati leo Blackburn inayoongozwa na Meneja Paul Ince aliewahi kuchezea Manchester United inakutana na timu ya Manchester United, Sir Alex Ferguson amekiri alimkosea Paul Ince pale alipomwita 'big-time Charlie' akimaanisha ni mtu hovyo, mpenda mzaha na asie na maana.
Bosi huyo wa Manchester United alitoa maneno hayo mwaka 1998 alipokuwa akiwapa nasaha Wachezaji wa Man U kabla ya pambano lao na Liverpool ambayo siku hiyo mmoja wa Wachezaji wao alikuwa Paul Ince.
Paul Ince aliuzwa kwa Inter Milan na Sir Alex Ferguson lakini alipohama Inter Milan akaenda kwa Watani wa Jadi wa Manchester United Klabu ya Liverpool kitendo ambacho kiliwakera sana washabiki wa Man U.
Sir Alex Ferguson amekiri: 'Najuta kutoa kauli ile. Lilikuwa kosa.'
Paul Ince alichukizwa sana na kitendo cha kuuzwa na Sir Alex Ferguson na akasusa kuongea na Ferguson kwa miaka kadhaa ingawa siku hizi wanaongea kama kawaida.
Maneno ya Ferguson kumdhihaki Paul Ince yalirekodiwa na Wapiga Picha za TV waliokuwa wanatengeneza filamu kuhusu Klabu ya Manchester United.
Leo Sir Ferguson anakutana uso kwa uso na Paul Ince kama Meneja wa Klabu kwa mara ya kwanza na Ferguson ametamka kwamba hakuwa na tatizo na Ince kama Mchezaji kwani alikuwa Mchezaji mzuri sana ingawa Washabiki wa Man U wanamchukia kwa kuhamia Liverpool.
Nae Paul Ince anasema: 'Kwa sasa nikiwa na matatizo huwa nampigia Sir Alex Ferguson kuomba mawaidha. Yeye ni mtu mwenye kiwango bora! Nimecheza chini ya Mameneja wengi lakini hakuna hata mmoja anaempata Ferguson!

No comments:

Powered By Blogger