Friday 3 October 2008

TIMU YA MARSEILLE YATEMBEZA KOFIA KIWANJA CHA NDEGE ILI WAPATE PESA ZA MAFUTA NDEGE IWARUDISHE KWAO!

Viongozi na Wachezaji wa Klabu ya Ufaransa Marseille walijkuta waking'uta mifuko yao ili kuchangishana pesa ili walipie mafuta ya ndege iliyokuwa iwarudishe kwao Marseille kutoka Madrid walikofungwa na Atletico Madrid mabao 2-1 kwenye mechi ya UEFA CHAMPION LEAGUE Jumatano usiku.
Mkasa huu uliwakuta baada ya ndege yao kunyimwa mafuta na Kampuni ya Mafuta CLH kwa madai hawakuruhusiwa na Exxon Kampuni ya Mafuta yenye mkataba na wamiliki wa ndege hiyo wa kuwajazia mafuta popote ndege zao zilipo duniani. CLH walidai Exxon haikutuma ombi lolote la mafuta kwao na wakagoma kutoa mafuta kwa mkopo wakidai pesa taslimu.
Ndipo kofia ikazungushwa kuchangishana EURO 3,000 za mafuta.
Kocha wa Marseille Eric Gerets alidhihaki mkasa huo kwa kusema: 'Ilibidi nitoe pesa zangu zote mfukoni na nikashindwa kununua hata sigara hapo uwanjani! Ingekuwa tumeshinda nisingejali! Lakini tumefungwa, tumekwama, sigara nimekosa, pesa sina!'

No comments:

Powered By Blogger