Tuesday 30 September 2008

REFA WA MAN U v BOLTON AOMBA RADHI KWA PENALTI TATA!

Refa Rob Styles aliechezesha mechi ya LIGI KUU Jumamosi huko Old Trafford kati ya wenyeji Man U na Bolton na kuipa Man U penalti baada ya kuhisi Ronaldo kafanyiwa madhambi [tizama picha] na Beki wa Bolton JLoyd Samuel ameomba radhi kwa Bolton kwa kutoa penalti hiyo kimakosa.

Kulikuwa na hisia baada ya kosa hilo Refa huyo atanyimwa kuchezesha LIGI KUU wikiendi inayokuja lakini Bodi ya Marefa imethibitisha kupitia Bosi wake Keith Hackett kuwa amepangiwa kuchezesha mechi kati ya Tottenham na Hull City. Imekuwa desturi Refa anaefanya kosa kubwa huwa hapangiwi mechi za LIGI KUU wikiendi inayofuata.

Mara baada ya mechi, Sir Alex Ferguson wa Man U alitania kuhusu penalti hiyo kwa kusema: 'Nilishangaa maana niliona mchezaji wao kacheza mpira! Lakini huyu Refa Rob Styles msimu uliopita alitunyima penalti 4 au 5 za wazi! Naona sasa anatulipa! Sasa tunamdai penalti 4!!'

Baada ya kuambiwa kuhusu Refa Rob Styles kuomba radhi, Sir Alex Ferguson aliunga mkono kwa kusema: 'Anastahili sifa kwa kuwa na ujasiri wa kukubali kosa. Ameungama na imeonyesha utu wake. Hili ni jambo bora sana kwa soka yetu.'
Baada ya mechi hiyo ya Jumamosi Meneja wa Bolton Greg Megson alilalamika vikali na kumtaka Refa Rob Styles aombe radhi.
Nae Nahodha wa Bolton Kevin Nolan amekaririwa akisema hata Wachezaji wa Man U hasa Ronaldo aliekuwa bado kalala kwenye nyasi baada ya 'rafu' hiyo alisikika akisema: 'Sitaki penalti!' wakati Darren Fletcher na Gary Neville walimwambia mara baada ya tukio hilo la rafu tata na kabla penalti kupigwa kwamba ile haikuwa penalti.
Penalti hiyo tata iliwapa Man U bao la kwanza kwenye dakika ya 60 na Rooney akaingizwa toka benchi na kufunga bao la pili.

No comments:

Powered By Blogger