Thursday 2 October 2008

CHELSEA WABANWA MBAVU RUMANIA

Wapigiwa wimbo wa Taifa wa Man United walipoingia uwanjani!!

Chelsea wameponea chupuchupu kufungwa huko Rumania walipokutana na timu mpya kwenye UEFA CHAMPIONS LEAGUE CFR Cluj na kulazimisha kutoka sare ya 0-0 kwenye mechi ya KUNDI A.
Ili kuwatia kiwewe Chelsea, wakati timu zikiingia uwanjani kwenda kukaguliwa, zilikaribishwa kwa ‘WIMBO WA TAIFA WA MANCHESTER UNITED’ uitwao ‘GLORY, GLORY MAN UNITED’ huku Washabiki wakilifungua bango kubwa lililoandikwa: ‘WARIDI NI JEKUNDU, CHELSEA NI BLUU, BIBI YANGU MZAA MAMA ANAPIGA PENALTI VIZURI KUPITA NYIE!’ wakiwadhihaki Chelsea waliposhindwa kwa penalti na Man United kwenye Fainali ya mashindano haya msimu uliopita.
Chelsea walipata pigo kwenye mechi hii baada ya Mshambuliaji wao wanaemtegemea Didier Drogba kuumia na kutolewa nje ya uwanja kwenye dakika ya 57.
CFR Cluj: Stancioiu, Tony, Souza, Cadu, Pereira, Culio, Muresan, Dani, Dubarbier, Yssouf Kone, Trica (Didi 88). AKIBA: Nuno Claro, Panin, Hugo Alcantara, Deac, Emmanuel Kone, Ruiz.
KADI: Pereira, Dani.
Chelsea: Cech, Bosingwa, Alex, Terry, Bridge, Mikel, Kalou (Anelka 46), Ballack, Lampard, Malouda (Di Santo 74), Drogba (Belletti 57). AKIBA: Hilario, Ivanovic, Ferreira, Stoch.
KADI: Alex, Anelka.
WATAZAMAJI: 22,000.
REFA: Florian Meyer (Germany).

LIVERPOOL WAENDELEZA USHINDI

Robbie Keane jana amefunga goli lake la kwanza kwa Liverpool tangu ahamie hapo kutoka Tottenham na kuiwezesha timu yake kushinda kwa mabao 3-1 kwenye mechi ya UEFA CHAMPIONS LIGI KUNDI D waliyocheza na PSV Eindhoven ya Holland Uwanja wa Anfield huko Liverpool.
Dirk Kuyt aliipatia Liverpool bao lakuongoza dakika ya 4 tu ya mchezo baada ya shuti la Fernando Torres kutemwa na Kipa Andreas Isaksson. Kabla ya haftaimu Robbie Keane akafunga bao la pili.
Nahodha Steven Gerrard akapachika bao la 3 kwa Liverpool katika dakika ya 74 na hilo likiwa goli lake la 100 kuifungia Liverpool.
PSV Eindhoven wakapata bao lao moja dakika nne baadae mfungaji akiwa Danny Koevermans.
Liverpool: Reina, Arbeloa, Skrtel, Carragher, Aurelio, Kuyt, Gerrard (Babel 81), Alonso, Riera (Benayoun 68), Torres, Keane (Leiva Lucas 75). AKIBA: Cavalieri, Dossena, Agger, Mascherano.
MAGOLI: Kuyt 5, Keane 34, Gerrard 76.
PSV: Isaksson, Kromkamp, Simons, Marcellis, Salcido, Brechet (Pieters 46), Mendez (Dzsudzsak 76), Culina, Bakkal, Amrabat, Wuytens (Koevermans 60). AKIBA: Cassio, Rodriguez, Zonneveld, Nijland.
KADI: Marcellis.
GOLIs: Koevermans 78.
WATAZAMAJJI: 41,097
REFA: Felix Brych (Germany).
MATOKEO KAMILI:

KUNDI A
Bordeaux 1-3 Roma
CFR Cluj 0-0 Chelsea

KUNDI B
Anorthosis Famagusta 3-1 Panathinaikos
Inter Milan 1-1 Werder Bremen

KUNDI C
Shakhtar Donetsk 1-2 Barcelona
Sporting 2-0 Basle

KUNDI D
Atletico Madrid 2-1 Marseille
Liverpool 3-1 PSV

MECHI ZINAZOFUATA:

Jumanne, 21 Oktoba 2008

KUNDI E

Man U v Celtic

Villarreal v AaB,

KUNDI F

Bayern Munich v Fiorentina,

Steaua Bucuresti v Lyon,

KUNDI G

FC Porto v Dynamo Kiev,

Fenerbahce v Arsenal,

KUNDI H

Juventus v Real Madrid,

Zenit St Petersburg v BATE Borisov

Jumatano, 22 Oktoba 2008

KUNDI A

Bordeaux v CFR Cluj-Napoca,

Chelsea v Roma,

KUNDI B

Inter Milan v Anorthosis Famagusta,

Panathinaikos v Werder Bremen,

KUNDI C

Basle v Barcelona,

Shakhtar Donetsk v Sporting,

KUNDI D

Atletico Madrid v Liverpool

PSV v Marseille,

No comments:

Powered By Blogger