Friday 3 October 2008



MECHI ZA JUMAMOSI: Tathmini

Sunderland v Arsenal

Sunderland watakuwa uwanjani kwao Stadium of Light kuwakaribisha Arsenal ambao watakuwa kama mbogo waliojeruhiwa baada ya kufungwa na Hull City bao 2-1 wiki iliyokwisha.
Sunderland huenda wakawakosa Kiungo Liam Miller, Teemu Tainio, Phil Bardsley na Grant Leadbitter kwa kuwa ni majeruhi.
Arsenal, mbali ya majeruhi wa muda mrefu kina Tomas Rosicky, Amaury Bischoff na Eduardo, Wachezaji wote wako fiti.

TIMU:

Sunderland : Gordon, Fulop, Chimbonda, Ferdinand, Collins, McCartney, Diouf, Whitehead, Miller, Reid, Richardson, Malbranque, Henderson, Cisse, Murphy, Healy, Stokes, Chopra.

Arsenal : Almunia, Clichy, Toure, Gallas, Sagna, Nasri, Fabregas, Denilson, Walcott, Adebayor, Van Persie, Fabianski, Song, Djourou, Vela, Bendtner, Ramsey, Eboue, Silvestre.

REFA: Lee Mason (Lancashire)

West Brom v Fulham

West Brom wakiwa uwanjani kwao The Hawthorns watawakosa Kiungo Kim Do-Heon na Filipe Teixeira.
Nao Fulham huenda wakamkosa Bobby Zamora anaetatizwa na Flu wakati Andrew Johnson kafungiwa baada ya kula kadi nyekundu mechi iliyokwisha.

TIMU:

West Brom : Carson, Kiely, Zuiverloon, Hoefkens, Barnett, Donk, Olsson, Robinson, Morrison, Greening, Koren, Cech, Beattie, Moore, Miller, Valero, Bednar, MacDonald, Pele.

Fulham : Schwarzer; Pantsil, Hughes, Hangeland, Konchesky; Davies, Bullard, Murphy, Gera; Zamora, Seol, Zuberbuhler, Nevland, Dempsey, Andreasen, Kallio, Baird, Stoor, Gray.

REFA: Mark Halsey (Lancashire)

Wigan v Middlesbrough

Wigan watakuwa kwao JJB Stadium na Mchezaji pekee mwenye hatihati ya kutocheza ni Lee Cattermole wakati wapinzani wao Middlesbrough huenda wakacheza bila ya Beki Robert Huth.

TIMU:

Wigan : Kirkland, Melchiot, Boyce, Bramble, Figueroa, Valencia, Cattermole, Palacios, Kapo, Heskey, Zaki, Brown, Camara, De Ridder, Kilbane, Koumas, Kupisz, Scharner, Taylor, Pollitt, Kingson.

Middlesbrough : Turnbull, Jones, Hoyte, Wheater, Huth, Riggott, Taylor, Grounds, Digard, O'Neil, Aliadiere, Downing, Johnson, Shawky, Alves, Mido, Walker, Emnes, Craddock.

REFA: Martin Atkinson (Yorkshire)

Blackburn v Man Utd

Blackburn wakiwa kwao Ewood Park wanawakaribisha jirani zao Mabingwa Manchester United.
Klabu hizi ziko umbali wa kiasi ya maili 50 kati yao.
Hii ni mechi ambayo Meneja wa Man U Sir Alex Ferguson anapambana na Mchezaji na Nahodha wake wa zamani ambae sasa ndie Meneja wa Blackburn Paul Ince.
Blackburn huenda wakawakosa kwa sababu ya maumivu Kipa Paul Robinson, Vince Grella na Benni McCarthy ingawa McCarthy ameshaanza mazoezi.
Kwa Manchester United, Wayne Rooney yuko kwenye hatihati baada ya kuumia enka juzi huko Denmark kwenye mechi ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE walipocheza na Aalborg wakati Paul Scholes, Owen Hargreaves na Michael Carrick kuna uhakika hawawezi kucheza.

TIMU:

Blackburn : Brown, Robinson, Bunn, Nelsen, Samba, Ooijer, Warnock, Emerton, Olsson, Tugay, Derbyshire, Santa Cruz, Villanueva, Fowler, Andrews, Fowler, Grella, Treacy, Pedersen.

Man Utd : Van der Sar, Amos, Neville, Brown, Rafael, Ferdinand, Vidic, Evans, Evra, Ronaldo, O'Shea, Fletcher, Anderson, Giggs, Nani, Tevez, Berbatov, Rooney, Welbeck.

REFA: ALAN WILEY (Stafforshire)

No comments:

Powered By Blogger