Monday 29 September 2008






MENEJA MPYA WA NEWCASTLE KUANZA KAZI AKIWA AMEKAA KWA WATAZAMAJI!

Joe Kinnear ambae ameteuliwa wiki iliyopita kuwa Meneja wa Muda wa Newcastle hadi mwisho wa mwezi wa Oktoba inapotegemewa Klabu huenda ikapata mmiliki mpya ataanza kazi yake kwa kukaa na Watazamaji badala ya benchi la Timu yake baada ya FA , Chama cha Soka Uingereza, kufafanua kuwa Meneja huyo bado hajatumikia adhabu aliyopewa mwaka 2004 ya kufungiwa mechi mbili na hivyo kutokukaa benchi la timu.

Joe Kinnear alipewa adhabu hiyo mwaka 2004 alipokuwa Meneja wa Nottingham Forest baada ya mechi waliyofungwa na Gillingham alipomwita Refa wa mechi hiyo 'ze comedy' yaani Msanii Mwigizaji na Mchekeshaji!

Wakati huo Kinnear alijitetea kuwa aliuliza: 'Huyu Refa anafanya shughuli gani na nikaambiwa ni Mwigizaji/Mchekeshaji basi nikaamua kumwita jina la 'COCO' yule Mchekeshaji maarufu!'

Tangu wakati huo mwaka 2004 Joe Kinnear alikuwa nje ya soka hadi wiki iliyopita.

Hivyo FA imetamka kifungo chake kimeanza kwa mechi ya Jumamosi walipofungwa 2-1 na Blackburn na mechi ya pili atakayoikosa ni ya tarehe 5 Oktoba 2008 watakapocheza na Everton.

No comments:

Powered By Blogger