Wednesday 1 October 2008

AaLBORG 0 MAN U 3

Dimitar Berbatov jana alifungua akaunti yake ya magoli kwa Man U alipopachika mabao mawili katika kipindi cha pili kwenye mechi ya michuano ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE iliyochezwa Denmark zidi ya wenyeji Aab Aalborg ambayo Man U walishinda kwa mabao 3-0.

Bao la kwanza la Man U lilifungwa na Wayne Rooney kwenye dakika ya 22 baada ya pasi tamu ya Ryan Giggs alieingizwa dakika chache kabla baada ya Paul Scholes kuumia goti.

AaB Aalborg: Zaza, Bogelund, Olfers, Beauchamp (Caca 38), Pedersen, Augustinussen, Risgaard, Curth, Johansson, Enevoldsen, Saganowski. AKIBA: Stenild, Due, Braemer, Sorensen, Kristensen, Ronnie Schwartz Nielsen.
KADI: Johansson, Zaza.
Man Utd: Van der Sar, Rafael Da Silva (Brown 66), Ferdinand, Vidic, Evra, Ronaldo, Scholes (Giggs 16), O'Shea, Nani, Berbatov, Rooney (Tevez 59). AKIBA: Amos, Anderson, Park, Evans.
KADI: Rafael Da Silva.
MAGOLI: Rooney 22, Berbatov 55, 79.
WATAZAMAJI: 10,346
REFA: Olegario Benquerenca (Portugal
).

ARSENAL 4 FC PORTO 0

Arsenal wakiwa nyumbani Emirates Stadium walianza mechi hii kwa kukoswakoswa pale FC Porto, Mabingwa wa Ureno, pale Mchezaji wao Cristian Rodriguez alipopiga kichwa kilichogonga mwamba na kufuatiwa na shuti la Lisandro lililoondolewa kwenye mstari wa goli likiwa tayari kutinga wavuni.

Arsenal wakazinduka na kupachika mabao mawili kupitia kwa Van Persie dakika ya 31 na Adebayor dakika ya 40 hivyo kwenda haftaimu wakiwa mbele kwa mabao 2 kwa 0.

Kipindi cha pili wafungaji haohao wakaongeza mabao mengine mawili wakati Van Persie alipopachika dakika ya 48 na Adebayor akafunga penalti dakika ya 71.

Arsenal: Almunia, Sagna, Toure, Gallas, Clichy, Walcott (Vela 71), Fabregas, Denilson, Nasri (Eboue 64), Van Persie (Bendtner 64), Adebayor. AKIBA: Fabianski, Ramsey, Silvestre, Djourou.
KADI: Clichy.
MAGOLI: Van Persie 31, Adebayor 40, Van Persie 48, Adebayor 71 pen.
FC Porto: Helton, Sapunaru, Bruno Alves, Rolando, Benitez, Guarin, Costa, Fernando (Lucho Gonzalez 46), Raul Meireles (Hulk 64), Rodriguez (Candeias 79), Lopez. AKIBA: Nuno, Pedro Emanuel, Stepanov, Lino.
KADI: Costa.
Att: 59,623
REFA: Herbert Fandel (Germany).


MATOKEO KAMILI:

KUNDI E

Aalborg 0 v Man U 3

Villarreal 1 v Celtic 0

KUNDI F

Bayern Munich 1 v Lyon 1

Fiorentina 0 v Steau Bucharest 0

KUNDI G

Arsenal 4 v Porto 0

Fenrbahce 0 v Dynamo Kiev 0

KUNDI H

Bate 2 v Juventus 2

Zenit St Petersburg 1 v Real Madrid 2

No comments:

Powered By Blogger