Friday 3 October 2008

Mchezaji Etxeberria asaini mkataba kuchezea Athletic Bilbao bure!!!!

Joseba Etxeberria amesaini nyongeza ya mkataba wa mwaka mmoja kuichezea Klabu ya Spain Athletic Bilbao iliyoko La Liga huko Spain bure bila ya kulipwa hata senti mmoja ikiwa pamoja na kutopokea mshahara hadi mkataba utakapoisha mwishoni mwa msimu ujao.
Mchezaji huyo wa wa zamani wa Kimataifa wa Spain ambae ni Kiungo mwenye umri wa miaka 31 alijiunga na Athletic Madrid akiwa na miaka 17 na hajahama tangu wakati huo. Mkataba wake wa kawaida wenye malipo kama ilivyo desturi uliisha mwishoni mwa msimu uliopita.
Ili kutimiza ndoto yake ya kustaafu akiwa Klabu moja tu na kuweka rekodi ya kucheza mechi 500 baada ya kuwa na Atletic Bilbao ndio maana Joseba Etxeberria amekubali kucheza bure kwa mwaka mmoja.
Mchezaji huyu alikuwa kwenye kikosi cha Spain cha Kombe la Dunia mwaka 1998 na ameshachezea Spain kwenye Fainali za Mataifa ya Ulaya mara mbili.
Rais wa Klabu hiyo Atletic Madrid Fernando Garcia Macua amesema: "Sisi kama Klabu hatuna jinsi ya kumshkuru!! Hiki ni kitendo cha upendo na uzalendo wa hali ya juu!!'
Nae mdau mmoja alinena: 'Kitendo hiki kinawaaibisha wale Mastaa wote wa sasa wenye uroho wa mabilioni ya pesa na hawana msaada kwa yeyote!!'

No comments:

Powered By Blogger