Friday 3 October 2008

Van der Sar arudi kuiokoa kwa muda Timu ya Uholanzi yenye majeruhi baada ya kustaafu.

Kipa wa Manchester United Edwin van der Sar ambae alitangaza kustaafu kuichezea Timu ya Taifa ya Uholanzi mara baada ya mashindano ya EURO 2008 mwezi Julai atarudi tena kuichezea Timu hiyo kwa mechi mbili tu wiki ijayo kwenye mapambano ya mtoano wa kuwania nafasi za kuingia FAINALI KOMBE LA DUNIA AFRIKA KUSINI 2010.
Kocha wa Uholanzi Bert van Marwijk na msaidizi wake Frank de Boer imebidi wamuombe Edwin van der Sar arudi kibaruani toka kwenye kustaafu kufuatia kuumia kwa Makipa wote wawili wa Timu ya Taifa.

Makipa hao majeruhi ni Maarten Stekelenburg wa Ajax na yule wa Feyenoord Henk Timmer.
Kocha Bert van Marwijk amemtaja Van der Sar kwenye kikosi cha Wachezaji 22 kitakachocheza mechi za KUNDI LA 9 na Iceland mjini Rotterdam, Uholanzi tarehe 11 Oktoba na ugenini zidi ya Norway siku nne baadae.
Van der Sar ameshaidakia Uholanzi mara128.

No comments:

Powered By Blogger