Wednesday 1 October 2008


MECHI ZA LEO:
Jumatano, 1 Oktoba 2008 [saa 3 dak 45 usiku saa za bongo]

KUNDI A

CFR Cluj-Napoca v Chelsea

Bordeaux v Roma

KUNDI B

Anorthosis Famagusta v Panathinaikos

Inter Milan v Werder Bremen

KUNDI C

Shakhtar Donetsk v Barcelona

Sporting Lisbon v Basle

KUNDI D

Atletico Madrid v Marseille

Liverpool v PSV
TATHMINI:
Chelsea baada ya kupata ushindi mnono nyumbani Stamford Bridge walipowafunga Bordeaux bao 4-0 sasa watakuwa nchini Romania kupambana na timu mpya kwenye mashindano haya CFR Cluj-Napoca iliyofanya maajabu kwenye mechi ya kwanza ilipoifunga timu yenye uzoefu na ngumu Roma ya Italia nyumbani kwake.
Nao Liverpool baada ya kushinda ugenini kwa bao 2-1 zidi ya Marseille sasa itakuwa nyumbani Anfield kupigana kuendeleza wimbi la ushindi watakapocheza na PSV Eindhoven ya Uholanzi iliyofungwa nyumbani na Atletico Madrid.
Mechi nyingine tamu ni ile ya KUNDI B wakati INTER MILAN, Timu ya Kocha Jose Mourinho, itakapoikaribisha timu ngumu toka Ujerumani Werder Bremen.
Juzi, Inter Milan ilifungwa na watani wao AC MILAN kwenye mechi ya Ligi ya Italia SERIE A kwa bao 1-0 kwa bao la Ronaldinho na hicho kikawa kipigo cha kwanza kwa Jose Mourinho tangu atue Italia.
Katika mechi hiyo nae Mchezaji mwenye sifa mbaya duniani Marco Materazzi wa INTER MILAN alikula kadi nyekundu ingawa alikuwa hachezi kwani alikuwa mchezaji wa akiba kwenye benchi na alituhumiwa kumtukana Refa.

No comments:

Powered By Blogger