Friday 3 October 2008

SCHOLES NA FLETCHER WAONGEZA MIKATABA

Mabingwa wa LIGI KUU UINGEREZA NA ULAYA, Manchester United, leo wametangaza Wachezaji wao Paul Scholes na Darren Fletcher wameongeza mikataba yao.
Paul Scholes ameongeza hadi Juni 2010 na Darren Fletcher hadi Juni 2012.
Meneja wa Man U alipotangaza habari hizi alitamka: 'Scholes ni uthibitisho kwamba ukijitunza binafsi basi utadumu kwa muda mrefu kwenye klabu kubwa. Tizama Scholes yuko hapa tangu ana miaka 14 na sasa ana miaka 34! Nae Fletcher yuko hapa muda mrefu kama Giggs, Scholes na Wes Brown. Uvumilivu na uchezaji wake ni hazina kwetu!'
Wakitoa shukrani zao, Scholes alisema kwamba ni jambo kubwa kuongeza mkataba kwani ana nia kubwa ya kupata mafanikio zaidi ya msimu uliokwisha. Na Fletcher akaunga mkono kwa kutamka kuwa ukichezea klabu kubwa kama Man U hutaki kuhama na daima unataka kuchangia mafanikio.

No comments:

Powered By Blogger