Sunday 28 September 2008


LIGI KUU UINGEREZA:
WASEMAYO MAMENEJA WA TIMU VIGOGO BAADA YA MECHI ZA JANA:
-Sir Alex Ferguson wa Mabingwa Man U kuhusu penalti tata iliyowapa bao la kwanza kwenye mechi waliyowafunga Bolton 2-0 alisema kwa mzaha: 'Nilishangaa maana niliona mchezaji wao kacheza mpira! Lakini huyu Refa Rob Styles msimu uliopita alitunyima penalti 4 au 5 za wazi! Naona sasa anatulipa! Sasa tunamdai penalti 4!!'
-Arsene Wenger wa Arsenal baada ya kuadhiriwa uwanjani kwake Emirates na timu 'kibonde' Hull City iliyopanda daraja msimu huu kwa mara ya kwanza tangu ianzishwe kwa kufungwa bao 2-1 tena kwenye siku aliyokuwa akiadhimisha miaka 12 ya kuwa Meneja wa Arsenal. Wenger alihuzunika: 'Tulikuwa si waangalifu pengine moyoni tulijiamini tutashinda kwa vyovyote vile! Hull walijituma na sie tulikosa nafasi nyingi! Hata tungeshinda sina sababu ya kusherehekea miaka 12 hapa!!'
-Luis Felipe Scolari wa Chelsea walipoifunga Stoke City bao 2-0: 'Tunajiamini na timu inacheza vizuri ingawa si soka ya kupendeza!'
-Meneja wa Liverpool Rafael Benitez baada ya kuwafunga watani wa jadi Everton bao 2-0 uwanja wa Everton Goodison Park kwa mabao yaliyofungwa na Fernando Torres: 'Sifa si kwa Torres peke yake ni timu nzima kwani wamecheza vizuri kitimu!'

No comments:

Powered By Blogger