RATIBA YA KOMBE la UEFA CHAMPIONS LEAGUE
Kesho na Jumatano viwanja mbalimbali Ulaya vitawaka moto kwa kuzikutanisha Klabu mahiri Ulaya katika mechi za Makundi ya kugombea Kombe la Klabu Bingwa Ulaya-UEFA CHAMPIONS LEAGUE .
Mabingwa watetezi Manchester United walioko Kundi E watakuwa ugenini nchini Denmark kupambana na Aalborg. Katika mechi ya kwanza ya Kundi hili Man U walitoka suluhu na Villarreal huko Old Trafford.
Arsenal watakuwa nyumbani Emirates Stadium kupambana na FC Porto ya Ureno huku wakiomba dua safari hii wapate ushindi baada ya kunusurika kwenye mechi ya kwanza waliposawazisha bao dakika za mwisho walipocheza ugenini na Dynamo Kiev.
Chelsea baada ya kupata ushindi mnono nyumbani Stamford Bridge walipowafunga Bordeaux bao 4-0 sasa watakuwa nchini Romania kupambana na timu mpya kwenye mashindano haya CFR Cluj-Napoca iliyofanya maajabu kwenye mechi ya kwanza ilipoifunga timu yenye uzoefu na ngumu Roma ya Italia nyumbani kwake.
Nao Liverpool baada ya kushinda ugenini kwa bao 2-1 zidi ya Marseille sasa itakuwa nyumbani Anfield kupigana kuendeleza wimbi la ushindi watakapocheza na PSV Eindhoven ya Uholanzi iliyofungwa nyumbani na Atletico Madrid.
Jumanne, 30 Septemba 2008 [saa 3 dak 45 usiku saa za bongo]
KUNDI E
Aalborg v Man U
Villarreal v Celtic
KUNDI F
Bayern Munich v Lyon
Fiorentina v Steau Bucharest
KUNDI G
Arsenal v Porto
Fenrbahce v Dynamo Kiev
KUNDI H
Bate v Juventus
Zenit St Petersburg v Real Madrid
Jumatano, 1 Oktoba 2008 [saa 3 dak 45 usiku saa za bongo]
KUNDI A
CFR Cluj-Napoca v Chelsea
Bordeaux v Roma
KUNDI B
Anorthosis Famagusta v Panathinaikos
Inter Milan v Werder Bremen
KUNDI C
Shakhtar Donetsk v Barcelona
Sporting Lisbon v Basle
KUNDI D
Atletico Madrid v Marseille
Liverpool v PSV
No comments:
Post a Comment