Sunday 28 September 2008



WIGAN 2 MANCHESTER CITY 1

Wakiwa na Wachezaji watatu ambao wamo Timu ya Taifa ya Brazil, Manchester City walijikuta wakibebeshwa bao 2-1 na Wigan katika mechi ya LIGI KUU iliyochezwa nyumbani kwa Wigan JJB Stadium.

Manchester City wakiwa na Wabrazil wao Robinho, Elano na Jo walishindwa kufurukuta kwa timu ya Wigan iliyocheza nguvu kazi tangu dakika ya kwanza hadi mwisho huku Mshambuliaji wao toka Misri Amr Zaki bila shaka ndie Mchezaji Bora wa mechi.

Wigan walitangulia kupata bao la kwanza kupitia kwa Valencia aliefunga kwa shuti murua na Manchester City wakasawazisha kibahati baada ya mpira kumbabatiza beki wao Kompany na kutikisa nyavu kufuatia frikiki.

Lakini Amr Zaki aliwafungia Wigan bao la ushindi kwa penalti baada ya Palacios wa Wigan kuchezewa rafu na Javier Garrido wa Manchester City.

Kipindi cha pili ingawa mechi ilichangamka sana hakuna mabao mengine yaliyopatikana.

No comments:

Powered By Blogger