Wednesday 22 October 2008

Baada ya Man U na Arsenal kung'ara jana, leo Chelsea na Liverpool vitani!!

Jana Mabingwa watetezi Man U na Arsenal walifuzu kuzipa sifa Klabu za Uingereza sasa leo usiku ni zamu ya Chelsea ambao watakuwa kwao Stamford Bridge wakipambana na AS Roma ya Italy na Liverpool watakuwa wageni wa Atletico Madrid kwenye Uwanja wa Vicente Calderon.

ATLETICO MADRID v LIVERPOOL

Liverpool leo watashuka uwanjani bila ya Mfungaji wao bora Fernando Torres pamoja na Beki wa kati Martin Skrtel kwani wote ni majeruhi.
Kipa wa Liverpool Jose Reina, ambae baba yake mzazi alichezea Atletico Madrid, amewaonya Wachezaji wenzake kuhusu Atletico Madrid kwa kutamka: 'Wana mastaa hatari sana kama Diego Forlan, Sergio Aguero na Florent Sinama-Pongolle.'
Timu ya Liverpool inategemewa kuchaguliwa kutoka: Reina, Arbeloa, Carragher, Agger, Dossena, Pennant, Gerrard, Alonso, Riera, Keane, Kuyt, Lucas, Insua, Ngog, Benayoun, El Zhar, Mascherano, Cavalieri.

CHELSEA V AS ROMA

Majeruhi wa Chelsea ambao hawajacheza mechi kadhaa za hivi karibuni huenda leo wakapata namba na hao ni Deco, Joe Cole na Kipa Petr Cech.
Nao AS Roma wanategemewa kuwarudisha tena kikosini Philippe Mexes na Christian Panucci waliokuwa na kifungo cha mechi za huko Italia pamoja na Nahodha Francesco Totti aliefanyiwa opersheni ya goti ambae alianza kucheza mechi yake ya kwanza siku ya Jumapili walipofungwa 4-0 na Inter Milan.
Wachezaji watakaowakilisha Chelsea wanategemewa kuwa: Cech, Hilario, Cudicini, Ivanovic, Ferreira, Malouda, Obi, Deco, Kalou, Bosingwa, Terry, Lampard, Anelka, Belletti, Alex, Carvalho, Mancienne, Bridge, Di Santo, J Cole.

No comments:

Powered By Blogger