Wednesday 22 October 2008

BUNDUKI ZETU NDOGO HAZINA WOGA-Wenger adai!!!

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amekisifia kikosi chake chenye chipukizi wengi kilichowabamizi Fenerbahce jana kwenye pambano la UEFA CHAMPIONS LEAGUE kwa mabao 5-2.
Arsenal, wakicheza ugenini nchini Uturuki, walikuwa na Wachezaji wenye wastani wa umri wa miaka 22 uwanjani na vilevile walimuingiza Mchezaji mdogo kutoka Wales Aaron Ramsey mwenye miaka 17 na akamudu kupachika bao la 5.
Wenger alikipamba kikosi chake kwa kudai: 'Timu yetu ni changa lakini nasikia furaha kwa kuona tumeweza kuja hapa ugenini na kutawala mchezo! Kasi yetu, kuzunguka kwetu uwanjani na utalaam wetu ndio silaha yetu iliyotufanya tuimiliki gemu!'

Berbatov amchengua Ferguson!

Bosi wa Manchester United Sir Alex Ferguson amefurahishwa na uchezaji wa Mshambuliaji wake Dimitar Berbatov baada ya kufunga mabao mawili kati ya matatu katika ushindi dhidi ya Celtic hapo jana kwenye mechi ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE.
Sir Alex Ferguson alitamka: 'Ni kazi nzuri sana amefanya! Sasa anatuletea ustadi na utulivu kwenye mashambulizi! Bila shaka ushirikiano wake na Rooney na Tevez utaboreka zaidi!'
Berbatov alishindwa kufunga goli katika mechi zake nne za kwanza alizochezea Man U lakini sasa ameshafunga magoli matano katika mechi nne.

No comments:

Powered By Blogger