Friday 24 October 2008

UEFA CUP: Portsmouth wafa Ureno, Aston Villa washinda Uingereza!!

Baada ya kipigo cha Tottenham cha mabao 2-0 walichopewa na Udinese huko Italia, Portsmouth nao wameuawa huko Ureno na Klabu ya Braga iliyowabandika bao 3-0 wakati Aston Villa wakiwa nyumbani Uingereza wamejikongoja kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Ajax ya Uholanzi.
Portsmouth walijikuta wako nyuma bao moja pale frikiki ya Luis Aguiar ya umbali wa mita 30 kumhadaa Kipa David James na kutikisa nyavu.
Sekunde 90 tangu kipindi cha pili kuanza Wason Renteria wa Braga akapachika la pili na dakika chache kabla mechi kwisha Osorio Alan akaweka bao la 3.

Nao Aston Villa wakiwa uwanjani kwao Villa Park walianza mechi wakielemewa na Ajax lakini Nahodha Martin Laursen alifunga kwa kichwa cha nguvu kufuatia kona iliyochongwa na Ashley Young dakika ya 8.
Ajax waliendelea kutawala mechi na haikushangaza pale waliposawazisha kwenye dakika ya 22 kufuatia kona ya Urby Emanuelson kufungwa kwa kichwa na Thomas Vermaelen.
Lakini Aston Villa walipachika bao la pili na la ushindi dakika ya 45 baada ya kazi nzuri ya Ashley Young kumaliziwa vizuri na Gareth Barry.
MATOKEO YA MECHI NYINGINE ZA UEFA CUP ZA LEO:
AS Nancy 3 Feyenoord 0
CSKA Moscow 3 Deportivo la Coruna 0
Dinamo Zagreb 3 NEC 2
FC Copenhagen 1 St Etienne 3
Twente Enschede 1 Racing Santander 0
Galatasaray 1 Olympiacos 0
Heerenveen 1 AC Milan 3
Hertha Berlin 1 Benfica 1
MSK Zilina 1 Hamburg 2
Partizan Belgrade 1 Sampdoria 2
Schalke 04 3 PSG 1
Sevilla 2 Vfb Stuttgart 0
Rosenborg 0 Club Bruges 0

No comments:

Powered By Blogger