Sunday 19 October 2008

TUZO YA MCHEZAJI BORA ULAYA 2008 IITWAYO 'Ballon d'Or': LIGI KUU UINGEREZA ina Wachezaji 11 kati ya 30 wanaogombea!!!!!

Waendeshaji wa Tuzo ya 'Ballon d'OR', gazeti maarufu la soka liitwalo France Football Magazine, ambayo huzawadiwa kwa MCHEZAJI BORA WA ULAYA kila mwaka, wametangaza majina ya Wachezaji 30 wanaochezea Klabu mbalimbali Ulaya ambao watagombea zawadi hiyo.
Ballon d'Or maana yake ni MPIRA WA DHAHABU na ilianza kwa kutunukiwa kwa Wachezaji Bora Ulaya tangu mwaka 1956 na mwaka huo wa uzinduzi mshindi alikuwa Mchezaji mahiri sana wa Uingereza aliechezea Klabu ya Blackpool, Stanley Mathews.
Alieshinda tuzo hiyo mwaka 2007 ni Mchezaji wa AC Milan na Brazil, Kaka.
Kabla ya mwaka 2007, Mchezaji anaeweza kushinda tuzo hii ilikuwa ni lazima achezee Klabu iliyo Ulaya ambayo iko chini ya himaya ya UEFA na kabla ya 1995 ilikuwa ni lazima Mshindi awe ni Raia wa Nchi ya Ulaya.
Kati ya Wachezaji 30 watakaopigiwa kura na Waandishi wa Habari, Wachezaji 11 wanachezea LIGI KUU UINGEREZA na kati ya hao 11 watatu tu ndio Waingereza halisi kwa Uraia na ambao ni Wayne Rooney, Steven Gerrard na Frank Lampard.
SERIE A ya Italia ina Wachezaji watatu na LA LIGA ya Spain ina Washindani 11.
Mchezaji anaetegemewa sana kushinda Tuzo hii ya Ballon d'Or 2008 ni Cristiano Ronaldo wa Manchester United ambae pia ameshashinda Tuzo za Mchezaji Bora wa UEFA 2008 na LIGI KUU UINGEREZA.
Inategemewa Ronaldo atapata upinzani mkali kutoka kwa Mshindi wa tuzo hiyo 2007 Kaka wa AC Milan na Lionel Messi wa Barcelona.
Majina maarufu ambayo yamekuwa kama mtindo kila mwaka lazima yawepo kwenye listi hii, ambayo ni yale ya Thierry Henry na Ronaldinho, safari hii hayamo kabisa.

LISTI KAMILI [Klabu na Nchi wanazotoka]:

Emmanuel Adebayor (Arsenal), Togo; Sergio Aguero (Atletico Madrid), Argentina; Andrei Arshavin (Zenit St Petersburg), Russia ; Michael Ballack (Chelsea), Germany; Karim Benzema (Lyon), France; Gianluigi Buffon (Juventus), Italy; Iker Casillas (Real Madrid), Spain; Cristiano Ronaldo (Manchester United), Portugal; Didier Drogba (Chelsea), Ivory Coast; Samuel Eto'o (Barcelona), Cameroon; Cesc Fabregas (Arsenal), Spain; Fernando Torres (Liverpool), Spain; Steven Gerrard (Liverpool), England; Zlatan Ibrahimovic (Inter Milan), Sweden; Kaka (Milan AC), Brazil; Frank Lampard (Chelsea), England; Lionel Messi (Barcelona), Argentina; Pepe (Real Madrid), Portugal; Franck Ribery (Bayern Munich), France; Wayne Rooney (Manchester United), England; Marcos Senna (Villarreal), Spain; Sergio Ramos (Real Madrid), Spain; Luca Toni (Bayern Munich), Italy; Edwin van der Sar (Manchester United), Netherlands; Rafael van der Vaart (Real Madrid), Netherland; Ruud van Nistelrooy (Real Madrid), Netherlands; Nemanja Vidic (Manchester United), Serbia; David Villa (Valence CF), Spain; Xavi (FC Barcelone), Spain; Youri Zhirkov (CSKA Moscow), Russia.

No comments:

Powered By Blogger