Tuesday 21 October 2008

REFA ALIETOA PENALTI TATA KWA MAN CITY AKUBALI KUIANGALIA UPYA NA KUTOA UAMUZI WAKE!!

Refa Rob Styles, aliewapa Manchester City penalti tata dakika ya 13 tu ya mchezo na vilevile kumlima Beki wa Newcastle Habib Beye kadi nyekundu kwa tukio hilo ambalo marudio ya video yamedhihirisha Habib Beye alicheza mpira na hakumchezea faulo Robinho [pichani], amekubali kulitazama upya tukio hilo na kutoa uamuzi kama ni sahihi au alikosea.
Hatua hii ya Refa Rob Styles kupitia upya uamuzi wake imethibitishwa na Meneja wa Newcastle Joe Kinnear ambae amesema: 'Niliongea na Rob Styles na amekubali kuliangalia upya na kama akiona amekosea basi kadi nyekundu kwa Beye itafutwa. Sisi tunamshkuru kwani sote ni binadamu na huwa tunakosea. Kukubali umekosea ni ushujaa wa hali ya juu!'
Katika mechi hiyo ya jana licha ya kucheza Wachezaji 10 tangu dakika ya 13 na kufungwa bao hilo la penalti, Newcastle walikuwa wanaongoza hadi dakika ya 85 ndipo Man City wakasawazisha na mechi kuisha kwa mabao 2-2.
Nao FA wamethibitisha Kamati yao ya Nidhamu itapitia tukio hilo la Beye kulimwa kadi nyekundu na kuamua kuifuta au kuiacha hiyo kadi siku ya Alhamisi.

No comments:

Powered By Blogger