Thursday, 23 October 2008

UEFA CUP: Udinese 2 Tottenham 0

Tottenham, klabu ambayo iko mkiani LIGI KUU UINGEREZA, leo tena imebamizwa mabao 2-0 na Timu ya Italia, Udinese, kwenye mechi ya kugombea Kombe la UEFA.
Msimu wa Tottenham unaonyesha sasa klabu ipo majaribuni na sasa hata Wachezaji wameanza kunung'unika waziwazi kama alivyofanya Mchezaji David Bentley alielalamikia mwanzo mbovu wa Tottenham msimu huu hali iliyomfanya Meneja Juande Ramos amtoe kwenye kikosi cha leo.
Uwanjani mambo yaliendelea kwenda mrama pale Kipa wao Heurelho Gomes katika dakika ya 24 aliposhindwa kumiliki pasi aliyorudishiwa na Beki wake na katika kupapatika akamchezea rafu Fabio Quagliarella wa Udinese, Refa akatoa penalti iliyofungwa na Antonio Di Natale.
Balaa haikushia hapo.
Kiungo wao John O'Hara akachezea rafu mbili ndani ya dakika moja na kila rafu aliyocheza akazawadiwa kadi ya njano hivyo akatwangwa nyekundu na akatolewa nje ya uwanja.
Msumari wa mwisho kwa Tottenham uligongomezwa dakika ya 86 ya mchezo pale Pepe alipoifungia Udinese bao la pili.

No comments:

Powered By Blogger