Saturday 25 October 2008

Wenger amuwakia Nahodha wake Gallas kwa kupigwa picha naiti klabu usiku wa manane!!!

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amewaka na kudai picha aliyopigwa Gallas akitoka ndani ya naiti klabu huko London usiku wa manane huku ana sigara mdomoni haikubaliki kwa maadili ya klabu na atazungumza na kumpa onyo kali Nahodha wake.
'Nitazungumza nae!' Wenger amesesema. 'Ni lazima ajue wajibu wake kama Nahodha wa klabu!'
William Gallas ambae hajacheza mechi hivi karibuni baada ya kuumia paja amepona na anategemewa kucheza mechi na West Ham Jumapili.
Msimu uliopita Gallas alipondwa sana kwa kuonyesha tabia asiyostahili kwa Nahodha pale alipoamua kukaa chini katikati ya uwanja kwenye mechi waliyotoka sare na Birmingham wakati mpira unaendlea na wakati huo inasemekana Wenger alitaka kumnyang'anya Unahodha.

Real Madrid wabwaga manyanga kwa Ronaldo!

Rais wa Real Madrid Ramon Calderon amesema klabu yake haina haja tena ya kumnunua Cristiano Ronaldo kwani Manchester United hawataki kumuuza.
Ronaldo ana mkataba na Mabingwa wa Uingereza na Ulaya Manchester United unaoisha mwaka 2010.
Real Madrid walijaribu kumrubuni sana Ronaldo kabla msimu haujaanza na ilibidi Man U wawashitaki Real kwa FIFA.
Calderon amedai: 'Manchester United ni klabu kubwa duniani na hatutaki mzozo nao na wakisema hawauzi mtu basi huwezi kufanya kitu ni bora uliache hilo suala.'
Nae Sir Alex Ferguson ametamka waziwazi Owen Hargreaves hauzwi baada ya kuibuka minong'ono kwamba mchezaji huyo ni majeruhi muda mwingi basi ni bora auzwe.
Ferguson ametamka: 'Kwa ajili ya Hargreaves bora nitamke waziwazi hauzwi na wala hatujafikiria hilo!'
'Kwa sasa yuko kwenye matibabu na anendelea vizuri.' Ferguson aliongeza. 'Haya magazeti kutangaza anauzwa ni stori nzuri kwao kwa sababu tu kacheza mechi 2 tu msimu huu! Wanasahau msimu uliopita alitusaidia sana kushinda LIGI KUU na Ubingwa wa Ulaya!'
Tangu Hargreaves atue Man U akitokea Bayern Munich kwa dau la Pauni Milioni 18 ameandamwa na tatizo la goti linalopona na kurudi tena na amekosa mechi nyingi.

No comments:

Powered By Blogger