Sunday 19 October 2008

Hull City waifunga West Ham na kuchupa hadi nafasi ya 3

Leo, timu iliyopanda daraja msimu huu Hull City mbele ya mashabiki wake kwenye Uwanja wa nyumbani wa KC, imezidi kuchanja mbuga baada ya kuwafunga wazoefu wa LIGI KUU West Ham ambao sasa wako chini ya Meneja Gianfranco Zola bao 1-0 na hivyo kushika nafasi ya 3 katika msimamo wa LIGI KUU.
Mpaka sasa, Hull City wamecheza mechi 8 na wana pointi 17, Arsenal wako wa 4 wakiwa wamecheza mechi 8 na wana pointi 16 huku Mabingwa Man United wako wa 5 na wana pointi 14 kwa mechi 7 walizocheza.
Hii ni mechi ya tatu mfululizo kwa Hull City kushinda ingawa mbili za kabla walishinda ugenini baada ya kuzipiga Arsenal 2-1 na Tottenham 1-0.
Mpaka mapumziko mechi ilikuwa dro na West Ham ndio waliotawala na kukosa mabao mengi.
Dakika tano tu ya kipindi cha pili, kona iliyopigwa na Andy Dawson ilitua kichwani kwa Michael Turner aliefunga bao la ushindi.

No comments:

Powered By Blogger