Tuesday, 21 October 2008

MAN U na ARSENAL wanashuka dimbani leo kwenye UEFA CHAMPIONS LEAGUE

Leo, katika michuano ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE, Mabingwa wa Kombe hilo, Mancheter United, wanawakaribisha Old Trafford wajomba zao Celtic ambao ni Mabingwa wa Scotland katika mechi iliyobatizwa 'Mapigano ya Uingereza'.
Huko Uturuki, Arsenal watakuwa wageni wa Fenerbahce katika mechi itakayokuwa ya vuta ni kuvute kwani daima timu za Kituruki huvimba sana wakiwa nyumbani kwao.
Katika mechi iliyopita, Manchester United waliwafunga Aalborg ya Denmark hukohuko Denmark kwa mabao 3-0 wakati Arsenal walipata ushindi uwanjani kwake Emirates walipoibandika FC Porto ya Ureno mabao 4-0.
Kikosi cha Arsenal leo kitashuka bila ya Kolo Toure, William Gallas na Bacary Sagna ambao wote ni majeruhi.
Kikosi cha Arsenal kinatazamiwa kuwa: Almunia, Song, Silvestre, Clichy, Eboue, Fabregas, Denilson, Nasri, Diaby, Walcott, Van Persie, Adebayor, Fabianski, Vela, Ramsey, Gibbs, Hoyte, Bendtner, Djourou.
Nao Manchester United watawakosa Paul Scholes, Owen Hargreaves, Michael Carrick na Patrice Evra kwani wote ni majeruhi.
Meneja wa Man U Sir Alex Ferguson amedokeza pia huenda akampumzisha Ronaldo na kumchezesha Nani badala yake ingawa hakuthibitisha kwa hilo.
Kikosi cha Man U kitatokana na: Van der Sar, Kuszczak, Brown, Neville, Rafael, Ferdinand, Vidic, Evans, O'Shea, Ronaldo, Nani, Fletcher, Anderson, Giggs, Gibson, Park, Tevez, Berbatov, Rooney, Manucho.
Nao Celtic watashusha kikosi kutoka kwa: Boruc, Caldwell, Wilson, McManus, Loovens, Naylor, McGeady, S Brown, Hinkel, Hartley, Robson, McDonald, Sheridan, Maloney, M Brown, McCourt, Hutchinson, Nakamura, O'Dea.

No comments:

Powered By Blogger