Sunday 19 October 2008

STOKE CITY 2 TOTTENHAM 1

Bila shaka Meneja wa Tottenham Juande Ramos kijasho chembamba kinamtoka baada ya kupata kipigo kingine kwenye LIGI KUU na hivyo kuzidi kuipigilia misumari timu yake inayoshikilia mkia kwenye ligi baada ya kufungwa mabao 2-1 na Stoke City timu iliyopanda daraja msimu huu.
Mbali ya kipigo kwa Juande Ramos, vilevile Wachezaji wake wawili Gareth Bale na Michael Dawson, walibandikwa kadi nyekundu na mwingine Vedran Corluka ilibidi akimbizwe hospitali kwa ambyulensi baada ya kuumizwa kichwani tukio lililofanya mechi isimame kwa dakika 11.
Katika historia ya Tottenham, huo ndio mwanzo mbaya kabisa wa msimu kwani baada ya mechi 8 wameambulia pointi 2 tu na wako wa mwisho kabisa.

No comments:

Powered By Blogger