Wapinzani wa mjini London wanakutana Stamford Bridge Jumapili na ushindi kwa wenyeji Chelsea utawafanya waongoze LIGI KUU UINGEREZA huku wamewatupa Arsenal pointi 13 nyuma.
Chelsea walitoka sare ya 0-0 na Newcastle hapo kwao Stamford Bridge wiki iliyokwisha kwenye mechi ya LIGI KUU wakati Arsenal alikula kipigo chake cha pili mfululizo kwenye LIGI KUU aliposhindiliwa 3-0 na Manchester City mjini Manchester uwanjani City of Manchester.
Kabla ya kipigo hicho, Arsenal aliadhiriwa kwa mabao 2-0 mbele ya mashabiki wake nyumbani kwake Emirates Stadium alipofungwa na Aston Villa pia kwenye mechi ya LIGI KUU kikiwa ni kipigo chake cha 5 msimu huu ambao mpaka sasa washacheza mechi 14.
Arsenal kwa sasa wanaenda mrama hata nje ya uwanja kwa migogoro ambayo imesababisha Nahodha William Gallas avuliwe madaraka na kiungo kijana mdogo wa miaka 21 Cesc Fabregas apewe madaraka hayo huku mashabiki nje ya uwanja wakianza kunung'unika waziwazi kitu ambacho hakijatokea katika utawala wa Meneja Arsene Wenger wa miaka 12 sasa.
Michael Barrack, Mjerumani kiungo wa Chelsea ambae majuzi tu alitamka Ubingwa msimu huu ni vita kati ya timu yake Chelsea na Man U, ametamba: 'Kwa sasa tunaongoza ligi na wao Arsenal wako nyuma yetu pointi 10. Kwa sasa wao si timu ngumu na nzuri kwani wana matatizo makubwa! Nia yetu ni kuwafunga na kuwaacha kwa pointi 13. Kila mtu hapa Chelsea ana njaa ya Ubingwa na hii unaihisi kwenye mazoezi!'
WAFUNGAJI BORA LIGI KUU UINGEREZA:
Nicholas Anelka wa Chelsea ndie anaeongoza kwa kufunga mabao mengi LIGI KUU kwa kufunga mabao 12 na nafasi ya pili imeshikiliwa na Wachezaji watatu waliofunga mabao 8 kila mmoja. Wachezaji hao ni Mfungaji Bora msimu uliopita Cristiano Ronaldo wa Man U ambao ndio Mabingwa LIGI KUU, Robinho wa Man City na Amr Zaki, Mmisri anaechezea Wigan.
Nafasi ya tatu imeshikwa na Agbonlahor wa Aston Villa na Darren Bent wa Tottenham kwa mabao 7 kila mmoja.
Nafasi ya 4 ni ya Defoe [Portsmouth], Geovanni [Hull City] na Ireland [Man City] wenye mabao 6 kila mmoja.
Nafasi ya 5 imeshikwa na Wachezaji 6 wenye bao 5 kila mmoja yaani Adebayor [Arsenal], Carew [Aston Villa], Cisse [Sunderland], Crouch [Portsmouth], Fuller [Stoke] na Kuyt [Liverpool].
No comments:
Post a Comment