Thursday 27 November 2008

Liverpool asonga mbele, Chelsea bado asota!!!!

Timu 13 zishaingia Raundi ya Mtoano ya jumla ya Timu 16.

Tatu zilizobaki ni ama Panathinaikos au Anorthosis Famagusta na mbili kati ya Chelsea, AS Roma au Bordeaux!!!

Kufuatia mechi za jana za UEFA CHAMPIONS LEAGUE, Timu za Liverpool, Mabingwa wa Italia Inter Milan na Atletico Madrid ya Spain wameungana na Timu nyingine 10 kuingia Raundi nyingine ya Mtoano ya Kombe hilo linalotoa Klabu Bingwa Ulaya.
Raundi inayokuja ya Mtoano itakuwa na jumla ya Timu 16 na droo yake kuamua timu ipi inakutana na ipi itafanyika tarehe 19 Desemba 2008 na mechi zenyewe za Raundi hiyo zitachezwa tarehe 24 na 25 Februari 2009 na marudiano tarehe 10 na 11 Machi 2009 kwa mtindo wa nyumbani na ugenini huku timu zitazoshinda Raundi hiyo zitaingia Robo Fainali.
Mpaka sasa Timu zilizofuzu kuingia Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ni pamoja na hizo zilizofuzu jana, yaani Liverpool, Inter Milan, Atletico Madrid, zitakazojumuika na Mabingwa Watetezi wa Kombe hili, Manchester United pamoja na Villareal toka Kundi E, Barcelona na Sporting Lisbon kutoka Kundi C, Lyon na Bayern Munich Kundi F, Arsenal na FC Porto Kundi G na Juventus na Real Madrid Kundi H.
Timu nyingine 3 zitakazokamilisha idadi ya Timu 16 moja itatoka Kundi B ambako tayari Inter Milan kashafuzu ingawa jana alipigwa 1-0 nyumbani kwake na Panathinaikos.
Nafasi moja ya kusonga mbele na kujumuika na Inter Milan toka Kundi hili itaamuliwa katika mechi ya mwisho hapo tarehe 9 Desemba 2008 wakati Panathinaikos atacheza na Anorthosis Famagusta na mshindi ndie ataendelea.
Nafasi mbili za mwisho kukamilisha jumla ya Timu 16 ni za Timu za Kundi A ambamo kukiwa kumesalia mechi moja kwa kila Timu, AS Roma, ambae jana aliifunga CFR Cluj ya Romania mabao 3-1, anaongoza Kundi hili akiwa na pointi 9, Chelsea, ambae jana alitoka dro ya 1-1 na Bordeaux, ni wa pili akiwa na pointi 8 na Bordeaux wa tatu akiwa na pointi 7 huku CFR Cluj wa mwisho akiwa na pointi 4.
Katika mechi za mwisho, AS Roma anamkaribisha Bordeaux na Chelsea atakuwa nyumbani Stamford Bridge kupambana na CFR Cluj.

No comments:

Powered By Blogger