Thursday, 27 November 2008

MWENYEKITI WA ARSENAL AINGIA VITANI KUMTETEA WENGER!

Mwenyekiti wa Klabu ya Arsenal Peter Hill-Wood [kulia] ameziita taarifa kwamba wamepoteza imani kwa Meneja wao Arsene Wenger aliedumu miaka 12 sasa kuwa ni 'upumbavu'.
Kwa mara nyingine tena msimu huu Arsenal imeonekana dhaifu na kukosa uwezo wa kupigania Ubingwa wa LIGI KUU UINGEREZA kwani mpaka sasa baada ya kucheza mechi 14 imeshafungwa mechi 5 na Mapaparazi washaanza kushika bango kwamba ikiwa kikosi cha Wenger kisiposhinda Kombe lolote msimu huu basi mwanzo wa mwisho wa Mfaransa huyo umewadia.
Mara ya mwisho Arsenal kushinda LIGI KUU ilikuwa msimu wa 2003/04 ambao hawakufungwa hata mechi moja! Na Kombe lao la mwisho kuchukua ni la FA mwaka 2005 baada ya kutoka suluhu 0-0 na Man U na kushinda kwa penalti 5-4.
Lakini, Mwenyekiti wa Arsenal Peter Hill-Wood amezishambulia ripoti hizo na kusema Wenger amefanya mengi hapo na haiwezekani kamwe Bodi ya Wakurugenzi imgeuke.
'Ndio amefanya mengi sana na namuunga mkono.' Alisistiza Mwenyekiti huyo. 'Katika miaka 12 hapa amefanya kazi kubwa! Sasa tupo theluthi moja tu ya msimu na ndio tumepata matokeo matatu au manne mabaya. Ni upumbavu kuzungumzia yeye!'

No comments:

Powered By Blogger