Monday 24 November 2008

BALLACK: 'Msimu huu Bingwa ni Chelsea au Man U'

Michael Ballack wa Chelsea amesisitiza Ubingwa wa LIGI KUU msimu huu ni vita kati ya Klabu yake na Mabingwa Watetezi Manchester United.
Ballack amewapuuza Liverpool ingawa ndio kwa sasa ni vinara wa pamoja na Chelsea kwenye msimamo wa ligi huku timu zote hizo zimefungana kwa kuwa na pointi 33 baada ya mechi 14 huku Man U wako nafasi ya tatu wakiwa na pointi 25 kwa mechi 13.
Timu zote hizo tatu za juu zilitoka sare ya 0-0 kwenye mechi zao za ligi za wikiendi hii iliyopita na kwa sasa Chelsea anaongoza ligi kwa tofauti ya magoli.
Ballack ametamka:'Kila mtu anazungumzia juu ya Vigogo wanne wa ligi yaani Chelsea, Liverpool, Man U na Arsenal lakini kwa sasa Arsenal wamepoteza mwelekeo na wako nyuma sana! Liverpool wazuri lakini wao ni timu ya kucheza Ulaya tu kwenye LIGI YA MABINGWA YA UEFA kwa sababu wao mkazo wao ni mechi moja au mbili tu hawana ubavu wa kuhimili mechi nyingi! Ukitazama matokeo na vikosi vilivyopo Chelsea na Man U utajua timu hizo ndizo ngumu na ziko tafu kupita zote!'

No comments:

Powered By Blogger