Monday 24 November 2008

Gallas huenda akarudishwa kikosini kwenye mechi ya kesho na Dynamo Kyiv

Aliekuwa Nahodha wa Arsenal, William Gallas, ambae alivuliwa Unahodha na kutemwa kwenye kikosi kilichoenda Manchester kupambana na Manchester City Jumamosi na hatimaye kupata kipigo cha 3-0 huko, huenda akarudi uwanjani kama Mchezaji wa kawaida kesho kwenye mechi ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE dhidi ya Dynamo Kyiv itakayochezwa Emirates Stadium.
Inaaminika utepe wa Nahodha utaenda kwa Kipa Manuel Almunia kama ilivyokuwa kwenye mechi ya juzi na Man City au huenda akapewa Beki wa pembeni Gael Clichy.
Gallas alipata adhabu hizo baada ya kutoboa siri za mgogoro ndani ya Arsenal hadharani kitendo ambacho kimeiudhi Klabu.
Baada ya kipigo cha Jumamosi huko Manchester, Meneja Arsene Wenger aligoma kuzungumzia ishu ya Gallas ingawa alidokeza bado anaamini Mchezaji huyo ana nafasi kubwa kuendelea kuchezea Arsenal.
Siku ya Jumapili, Gallas alijumuika na Wachezaji wengine wenzake wa kikosi cha kwanza katika mazoezi ya kujitayarisha na mechi ya Dynamo Kyiv.

No comments:

Powered By Blogger