Wednesday, 26 November 2008

Ferguson: 'Rooney ameniomba radhi kwa kudanganya kaangushwa ndani ya boksi!'

Meneja wa Mabingwa wa Ulaya Manchester United Sir Alex Ferguson amesema Mchezaji wake Wayne Rooney alimtaka radhi kwa kugushi kachezewa rafu ndani ya penalti boksi na kujiangusha ili apate penalti katika mechi ambayo timu yake ilitoka suluhu 0-0 na Villareal jana kwanye mechi ya UEFA Champions League iliyochezwa uwanjani Estadio El Madrigal nchini Spain.
'Ameniomba radhi na kusema hakukusudia.' Ferguson alisema. 'Nadhani alikuwa amemtizama sana Robert Pires [mchezaji wa zamani wa Arsenal na sasa yuko Villareal]. Lakini, yeye ameomba radhi na huyo Pires hana hata haya, haombi radhi!'
Ferguson vilevile alizungumzia kuhusu rafu mfululizo anazofanyiwa Cristiano Ronaldo.
Alitamka: 'Ni mbinu za timu pinzani kumzuia mchezaji bora. Lakini Refa wa jana kutoka Italia Roberto Rosetti alikuwa mzuri na mkali kwa timu zote!'
Refa Roberto Rosetti alimpa Kadi Nyekundu Mchezaji wa Villareal Joan Capdevila na kumtoa nje kwa kumshindilia Ronaldo njumu juu ya goti zilizoacha alama pajani.

Wenger akiri ushindi finyu umewapa ahueni!!

Arsene Wenger amekiri ushindi finyu walioupata Arsenal jana ambao umewasaidia kufuzu kuingia Raundi inayofuata ya UEFA Champions League baada ya kuwachomeka Dynamo Kiev bao 1-0 unwanjani Emirates kwa bao la dakika ya 87 lililofungwa na Nicklas Bendtner umewapa ahueni kidogo kufuatia vipigo mfululizo kwenye LIGI KUU UINGEREZA hali iliyosababisha mtafaruku uliomfanya amtimue Nahodha wake William Gallas na kumpa Cesc Fabregas utepe huo.
Wenger alipumua kwa kusema: 'Ushindi huu umetutuliza kidogo! Gallas alicheza kwa moyo wote na Kepteni mpya Fabregas alihaha kila dakika!'

No comments:

Powered By Blogger